Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Falsafa makini Rummenigge amchambua Pep Guardiola

Muktasari:

  • “Kwa sababu moja au nyingine umakini wetu umeanguka katika wiki tatu zilizopita, pengine kushinda taji la ligi mapema kumeipunguzia kasi timu nzima au baadhi ya wachezaji wachache,’’ anasema Rummenigge.

KATIKA toleo lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, tuliona jinsi Mwandishi Marti Perarnau alivyozungumza na mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge ambaye alionyesha jinsi klabu ilivyo na matumaini na Pep na kugusia kiini cha matokeo mabaya kwa mtazamo wake. Sasa endelea…

“Kwa sababu moja au nyingine umakini wetu umeanguka katika wiki tatu zilizopita, pengine kushinda taji la ligi mapema kumeipunguzia kasi timu nzima au baadhi ya wachezaji wachache,’’ anasema Rummenigge.

“Hata hivyo, bado naamini hadhi na uwezo wa Pep kutekeleza majukumu yake vyote vinategemea namna ambavyo sisi tutakubaliana na falsafa zake, hatuhitaji kumwambia au vinginevyo, bali aendelee kuwa Pep yule yule kama alivyo,’’ anasema Rummenigge.

Baadaye mwandishi na mtunzi wa kitabu, Perarnau akamuuliza, vipi kuhusu kipigo Bayern ilichokipata katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, ni janga kubwa?

Rummenigge akajibu: “Siwezi kulipinga hilo na kwa mara ya kwanza nilimuona Pep akiwa ameadhibiwa vibaya katika mechi hiyo, yote kwa yote haya mambo huwa yanatokea na hiyo ni kwa sababu alibadili baadhi ya taratibu zake kwenye mbinu za kiuchezaji bila ya kuwa na uhakika wa asilimia 100.

“Alifanya uamuzi ambao kwa hakika haukuwa hasa ule wake uliozoeleka na yeye mwenyewe alichukizwa na kilichotokea kwa kushindwa kushikamana na mawazo yake, alikuwa wazi katika jambo hilo, alilipunguzia nguvu eneo la kati na kuamua kucheza soka la moja kwa moja, alijiruhusu kushawishika na matokeo ya mechi ya ugenini kule Bernabeu badala ya kizingatia kiwango cha Bayern ya wakati ule.

“Pamoja na yote hayo naweza kukwambia kitu, shutuma alizokumbana nazo siku ile haikuwa haki, alicheza mchezo ule kwa namna ile ile anavyoichukulia mechi katika kipindi chote cha msimu, alikuwa ni mwenye kuutafuta mpira, ni kweli kwamba hatukuweza kupata bao na ndio maana watu waliharakisha kumtupia shutuma.

“Kama tungecheza vilevile na kufunga bao kule Madrid kila mmoja angemwita Pep mtu mwenye akili za kiwango cha juu lakini ukweli baadhi yetu sisi ambao tumekuwa katika mchezo huu kwa muda mrefu hatujiruhusu kucheza tukiwa wenye kushawishiwa na matokeo ya hapa au kule (nyumbani au ugenini) badala yake ni lazima pia kuufanyia tathmini ya kina mchezo.

“Kama Gotze angefunga bao katika mechi ile ya Bernabeu, Bayern na Pep wangekuwa wakipongezwa mwanzo mwisho lakini alishindwa kufunga na mwisho ya yote ikawa ni msiba.

“Hapa Ujerumani tuna tatizo hatuweki mkazo zaidi kwenye aina ya mbinu za kiuchezaji, tumeridhika kwa kucheza kwa kasi, kutumia nguvu na kucheza soka la moja kwa moja, lakini soka ni zaidi ya hilo. Tunayo sababu ya kushinda taji la ligi kwa kuongoza kwa mbali na sababu hiyo ni Pep,” anasema Rummenigge.

Baada ya ufafanuzi huo wa Rummenigge, Mwandishi Perarnau akamuuliza, Pep ana miaka miwili zaidi katika mkataba wake, unatarajia nini kwake kwa wakati huu?

Rummenigge anajibu: “Naamini anaweza kubadili utamaduni wa soka la Ujerumani bila kujali nini kimetokea katika wiki tatu zilizopita pamoja na ukweli baadhi ya watu tayari wameanza kumshusha thamani yake na kile alichokifanikisha hadi sasa.

“Mawazo ya watu ambayo yamemuunga mkono muda mrefu, ghafla yamebadilika na kuwa ya kumkatisha tamaa na kumshusha hadhi yake huku zikiibuka hoja falsafa zake si nzuri kiasi hicho, kwangu mimi kinyume chake ndio ukweli. Nimezungumza na wachezaji walio hapa kwa muda mrefu, ambao wamekuwa na makocha watano hadi saba katika miaka mingi waliyokuwa hapa, na wote wanasema kitu kimoja, Pep yuko juu na wanamuunga mkono. Ameleta mawazo mengi mapya, kocha ana hadhi yake mbele ya wachezaji anaowaongoza.

Itaendelea Jumanne ijayo…