Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali CAF Yanga akili kubwa, yapewa mwamuzi wa Simba

YANGA wanaelekea kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algier, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga wanakwenda kwenye fainali hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kushiriki fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika tangu limeanzishwa, lakini ikiwa inapewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa huo.

Yanga wameweka mikakati sawa kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo, lakini moja ya jambo walilofanya ni kuhakikisha kuwa mchezo unapigwa majira ya saa 10 jioni jambo ambalo limeshafanikiwa, lakini kubwa kuliko yote ni ulinzi kwenye kambi yao na kuhakikisha hakuna mtu yoyote nje ya wahusika anayeruhusiwa kuingia.

"Kuna mambo mengi tumeyafanya, lakini ukweli ni kwamba tumekuwa tukifanya mambo mengi kuhakikisha kuwa tunapata ushindi kwenye mchezo huu muhimu kwa ajili ya Watanzania wote, tumejidhatiti kwenye kila eneo, lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha kila mchezaji anakuwa kwenye utulivu wa hali ya juu kambini," kilisema chanzo hicho baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Singida wa nusu fainali ya Kombe la Azam Federation.

Taarifa hiyo inasema kuwa Yanga wameboresha ulinzi wa kutosha kwenye kambi yao na hawataki kuona mtu yoyote ambaye siyo mhusika akiwa kwenye eneo la kambi hiyo iliyopo AVIC Town Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na hata baadhi ya viongozi wa timu hiyo.

"Ukweli ni kwamba timu inahitaji utulivu wa hali ya juu, hakuna mtu anayeruhusiwa kwenda kambini kufanya kikao, au kuzungumza jambo lolote na wachezaji nje ya kocha na benchi lake la ufundi, hii ni kwa kuwa mwalimu anataka kila mchezaji awe kwenye umakini mkubwa.

"Lakini pia kwa wachezaji nao hakuna anayeruhusiwa kutoka kambini, tukishaingia ndani kila kitu kinakuwa ni ndani tu hadi mwisho wa mchezo hapa, ambapo watapata siku moja ya mapumziko na baada ya hapo timu itaondoka kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa fainali ya pili.

Hata hivyo, chanzo hicho kimesema kuwa utaratibu wa bonasi ya mchezo huo bado haujapitishwa lakini uhakika ni kwamba kiwango cha chini kabisa kwenye mchezo huo kitakuwa shilingi milioni 500.

"Unajua kiwango cha nyuma ilikuwa milioni 400, hivyo naamini kuwa fainali lazima iwe juu zaidi kwa kuwa huu mchezo una umuhimu mkubwa zaidi, hivyo tunaamini kiwango cha chini itakuwa milioni 500 ingawa inaweza kuzidi hapo," kilisema chanzo hicho.

Mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho Afrika wa Yanga dhidi ya USM Alger utaamuliwa na refa, Jean-Jacques Ndala Ngambo raia wa DR Congo.

Yanga na USM Alger zitacheza mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho, Mei 28 kisha zitarudiana Juni 3, mechi itakayochezwa nchini Algeria.

Mwamuzi huyu mwenye umri wa miaka 35, ni kati ya waamuzi wazoefu akichezesha mechi 34 za mashindano ya Caf, tangu mwaka 2017, lakini akiwa na uzoefu mkubwa na mechi za Simba.

Ngambo kwenye mechi hizo ameonyesha kuwa sio refa wa masihara kwani kwenye suala la kutoa kadi kwake ni jambo la kawaida hivyo wachezaji wa Yanga na Algers wanatakiwa kuwa makini zaidi.

Katika mechi hizo Ngambo ametoa kadi za njano jumla 98, huku kadi nyekundu akitoa tatu tu.

Ngambo kwenye mechi moja ya Ligi ya Mabingwa kati ya RS Berkane dhidi ya Hassania Agadir ambayo Berkane ilishinda 2-1, alitoa kadi nane za njano.

Mchezo mwingine ambao alitoka kadi nyingi za njano ni kwenye Ligi ya Mabingwa ambao Simba ilishinda 2-1 dhidi ya RSB Berkane na alitoa kadi saba za njano.

Mwamuzi huyu pia ni kama vile ana kismati na timu za Tanzania kwani ameshachezesha mechi tatu za Simba huku mbili Simba ikifungwa na moja ikishinda.

Alichezesha mechi ya Simba ya kwanza kwenye Shirikisho dhidi ya Saoura ambayo Simba ilifungwa 2-0 mwaka 2019, na dhidi ya Galaxy Simba akipoteza 2-0 tena msimu uliopita.

Mchezo wa mwisho wa Simba kuchezesha ni kwenye Ligi ya Mabingwa ambao Simba iliifunga RS Berkane 1-0 msimu uliopita.

Mechi nyingine alizochezesha Recreativo do Libolo vs Zesco (njano nne, Ligi ya Mabingwa), Mamelod Sundowns vs Wydad Casablanca (alikaa mezani, Kombe la Shirikisho), Al Masry vs Songo (kadi ya njano moja, Ligi ya Mabingwa) na FC Platinum vs Al Ahly (kadi za njano tatu, Kombe la Shirikisho)

Wydad Casablanca vs Mamelodi Sundowns (kadi za njano nne,Kombe la Shirikisho), Etoile du Sahel vs Zamalek (kadi za njano tano, nyekundu moja, Ligi ya Mabingwa), RSB Berkane vs Gor Mahia (kadi za njano moja, Ligi ya Mabingwa) na Saoura vs Simba (Njano moja, kombe la Shirikisho).

Lobi Stars vs Wydad Casablanca (Kadi za njano nne, Kombe la Shirikisho), Orlando Pirates vs CARA Brazzaville (Njano moja, Ligi ya Mabingwa Afrika), Etoile du Sahel vs De Agosto (Kadi za njano mbili, kombe la Shirikisho) na Mamelod Sundowns vs Togo Port (Kadi ya njano moja, Kombe la Shirikisho).

Galaxy vs Simba (kadi za njano mbili, kombe la Shirikisho), Raja Casabalanca vs Kabylie (Muamuzi wa mezani, Ligi ya Mabingwa), Kaizer Chiefs vs Wydad Casablanca (kadi za njano tano, kombe la Shirikisho), Al Ahly vs RSB Berkane (Muamuzi wa mezani), Belouizdad vs Es Tunis (kadi za njano nne, kombe la Shirikisho), Zamalek vs Es Tunis (Kadi za njnao nne, Kombe la Shirikisho) na Petro de Luanda vs Wydad Casablanca (kadi za njano tatu, kombe la Shirikisho).

RSB Berkane vs Hassania Agadir (kadi nane za njano, Ligi ya Mabingwa), Al Ahly vs Mamelod Sundowns(kadi moja ya njano, kombe la Shirikisho), Al Nasry vs Horoya (kadi nne za njano, Ligi ya Mabingwa) na ES Tunis vs Kabylie (kadi nne za njano, kombe la Shirikisho).

Belouizdad vs Al Merreikh (kadi za njano sita, kombe la shirikisho), FAR Rabat vs Future (kadi tatu za njano, Ligi ya mabingwa), Mamelod Sundowns vs Al Hilal Omdurman (kadi za njano mbili na nyekundu moja, kombe la shirikisho), Cotonsports vs Royal Leopards (kadi mbili za njano, kombe la shirikisho) na Al Masr vs RSB Berkane (Muamuzi wa pembeni).

Zingine ni Al Ahly vs Raja Casablanca (kadi za njano sita na nyekundu moja, kombe la Shirikisho), Simba vs RSB Berkane (kadi za njano saba, Ligi ya mabingwa), Zamalek vs Petro de Luanda (kadi za njano tatu, kombe la shirikisho) na Al Ahly vs Raja Casablanca (kadi za njano nne, Caf Super Cup).