DStv yazindua promosheni mpya kwa mashabiki wa soka
Kaimu Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Shumbana Walwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
Dar es Salaam. Kampuni ya MultiChoice imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la TV ni DStv ambayo inatoa ofa kwa mashabiki wa soka wa ligi kubwa za Ulaya ambazo kwa sasa zinaelekea kufikia ukingoni.
Katika kuhakikisha kuwa mteja wa DStv hakosi kila aina ya burudani, DStv imejipanga kuhakikisha kuwa mteja wake anapata kila aina ya burudani ambapo wateja wapya kwa sasa wanapata seti nzima ya DStv kwa Sh 99,000 hii ikijumuisha na kifurushi cha Compact cha Sh56,000 bure.
Kaimu Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Shumbana Walwa amesema DStv imeongeza burudani kiasi kwamba unapozungumzia TV, unamaanisha DStv kwani ndipo zinapopatikana kila aina ya vipindi ikiwemo burudani, michezo, filamu, Habari, Makala na vipindi motomoto vya watoto.
“Tunaposema TV ni DStv, tunamaanisha kwani sasa mteja mwenye DStv nyumbani kwake anapata vipindi vya kila aina tena kwa gharama nafuu kulingana na uwezo wake kwani sasa vifurushi vyetu vinaanzia Sh 10,000 tu,” alisema.
Ametoa mfano kwa wapenzi wa soka ambapo wataendelea kushuhudia michuano ya Shirikisho ambapo timu ya Yanga imetinga nusu fainali, michuano ya ligi maarufu duniani kama EPL, La liga na Serie A bila kusahau michuano ya UEFA, EUROPA League, FA na mingineyo.
Washabiki na wapenzi wa michezo mingine nao hawajaachwa nyuma kwani michezo kama Basketball (NBA), Formula One, Mieleka, Ngumi, Tenis, Rugby, Cricket na mingineyo bado inaonekana kwenye kisimbuzi cha DStv.
Shangwe kubwa ni kwa wale wapenzi wa filamu za Bongo ambapo tamthilia maarufu kama Jua kali, Huba, Pazia bado zinazidi kupamba moto bila kusahau vipindi vingine kama Mwali, Mizani ya Ushambenga, Kitimtim, ICU, Ya Walimwengu Pamoja na vichekesho vya Orijino komedy na Watu baki vikiwa vinaendelea.
Shumbana amebainisha kuwa wakati burudani hii ikiendelea, wateja wa DStv wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu watatambulisha vipindi vipya na vya kusisimua ndani ya DStv ambapo wale wapenzi wa tamthilia, watakuwa na wakati mgumu kutoka majumbani mwao kwakuwa mzigo wa tamthilia na filamu utakuwa wa bandika bandua ndani ya DStv.
Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa DStv Tanzania Davis Mihyo amesema mbali na kuwahakikishia wateja wa DStv burudani wamejipanga kuwahudumia wateja kwa ufanisi mkubwa Zaidi. Amesema kuwa kwa sasa wana njia nyingi mbadala za wateja kujihudumia bila kulazimika kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja.