DStv yaja na ofa kabambe msimu huu wa sikukuu
Dar es Salaam. Kampuni ya DStv imezindua msimu wa sikukuu ambapo mteja akayelipia kifurushi chake atapandishwa na kuunganishiwa kifurushi cha juu yake kwa mwezi mzima bila malipo ya ziada.
Promosheni hiyo ya sikukuu inataajiwa kumalizika January 24 mwakani ina lengo la kuwapafaraja zaidi wateja kuangalia burudani mbalimbali baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.
Mkuu wa na thamani kwa wateja wa MultiChoice Tanzania Hilda Nakajumo amesema hata kama mteja kifurushi chake kilimalizika na alikuwa hajalipia, atapata ofa hiyo punde tu atakapohuisha kifurushi chake cha awali.
“Msimu huu wa sikukuu tunaileta familia ndugu na jamaa pamoja na ili kuhakikisha kuwa hawapungukiwi na burudani, tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe ili kuwawezesha kupata burudani ya hali ya juu kwa kufurahia chaneli nyingi Zaidi za DStv zikiwemo katuni kwa ajili ya Watoto, michezo, tamthilia, Habari na Makala mbalimbali” alisema Nakajumo.
Hilda alisema kuwa wateja wa Compact Plus atapandishwa mpaka kwenye kifurushi cha Premium hali kadhalika kwa vifurushu vingine.
“Kuna msimu mpya wa tamthilia pendwa ya The Good Doctor ndani ya M-Net pamoja na filamu maarufu kila Jumapili kama The King’s Man, The Bad Boys pamoja na Moonfall.
Pia kuna vipindi kama Real Housewives of Salt Lake City ndani ya 1Magic kuanzia tarehe 26 Disemba na pia atajionea msimu mpya wa The History of Christianity ndani ya chaneli ya Curiosity kuanzia tarehe 25 Disemba,” alisema.
Alisema kuwa wateja wa kufurushi cha Shangwe watapandishwa kwenye kifurushi cha Compact na kufuatilia vipindi kama The Best Man Holiday na kipindi maarufu cha Trevor Noah: Welcome to America pamoja na Mad Madea Week ndani ya Studio Universal.
“Msimu wa sikukuu familia nyingi zinakutana pamoja na hawa ndio wapenzi wetu. Tunataka wateja wetu washerehekee sikukuu kwa furaha zaidi kwa kupata burudani isiyokifani kupitia DStv. Kwakuwa msimu huu ni msimu wa kutoa, basi na sisi tumeona tutoe kwa wateja wetu ili waweze kuunganika na wapenzi wao kwa kutengeneza kumbukumbu pamoja na DStv” unapata huduma popote ulipo kipindi hiki cha sikukuu.