Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Droo ipo freshi, tutawaonyesha

DROO ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefanyika jioni hii kwa Yanga kutupwa Kundi D sambamba watetezi Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama, huku watani wao, Simba wakipangwa Kundi B pamoja na Wydad Casablanca ya Morocco, Asec Mimosas ya Ivory Coast na Jwaneg Galaxy ya Botswana.

Mabosi wa Yanga wamesema droo hiyo kwao wanaiona freshi tu, na wanaona ni kipimo kizuri cha kuthibitisha ubora kwenye michuano hiyo iliyotinga makundi baada ya kusota miaka 25 iliyopita.

Droo hiyo ya mechi za makundi zinazoanza Novemba 24 na kumalizika Machi mwakani, imefanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini huku Yanga ikipangwa kuanzia ugenini na kumalizia ugenini ilihali Simba itaanza na kumalizia mechi zake nyumbani.

Makundi mengine ni A lililo na timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, TP Mazembe ya DR Congo, Pyramids ya Misri na Nouadhibou ya Mauritania, wakati kundi C lina Etoile du Sahel ya Tunisia, Petro Atletico ya Angola, Al Hilal ya Sudan na Esperance ya Tunisia.

Ratiba zinaonyesha Yanga itaanzia ugenini kuvaana na CR Belouizdad kisha kuikaribisha Al Ahly, kabla ya kuifuata Medeama kwao Ghana na kurudiana wiki moja baadae na kisha kuwapokea Waalgeria na kwenda kumalizia mechi yake Cairo Misri dhidi ya watetezi wanaoshikilia rekodi ya kutwaa taji hilo mara 11.

Kwa upande wa Simba, itaanza mechi zake kwa kuikaribisha Asec Mimosas, kisha kuifuata Galaxy, kisha kuifuata Wydad itakayorudiana nao kwenye mechi itakayofuata kisha kuifuata Asec na kuja kuhitimisha na Galaxy na timu mbili za kila kundi zitapenya kwenda robo fainali ya michuano hiyo.

Wakizungumzia droo hiyo na makundi ilizopangwa timu zao, mabosi wa Simba na Yanga wamesema wanaona freshi tu, kwani huu ndio wakati wa kuonyesha ubabe wao mbele ya wapinzani ili zivuke kwa pamoja kwenda robo fainali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amesema wapo tayari kwa kibarua kilicho mbele yao.
"Hakuna kundi rahisi katika haya mashindano. Hizo timu zote kwenye kundi letu zilishawahi kutufunga na sisi tulishawafunga.

Kundi ni gumu hivyo tunahitaji kufanya kazi hasa tuweze kufanya vizuri na kutimiza malengo yetu," amesema Try Again, huku Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amefunguka kuwa, wapo tayari kupambana na wapinzani wao kwenye kundi walilopo.

"Ukiwa mfuatiliaji wa soka utabaini kwamba kundi A na D ndio makundi magumu. Tupo dhidi ya timu ngumu lakini hii ndio hatua ya kuitambulisha Yanga. Naamini tukishirikiana vyema tutafanya vizuri," amesema Kamwe na kuongeza;

"Huu ndio wakati mzuri na kipimo kizuri kwa Yanga kuonyesha tulipo baada ya kutinga makundi iliyoisotea kwa miaka 25. Ni nafasi ya kwenda kujipima uwezo wa klabu hiyo kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika."

Kundi D

        P    W    D    L    F    A    PTS
1. Al Ahly        0    0    0    0    0    0    0
2. CR Belouizdad    0    0    0    0    0    0    0
3. Yanga        0    0    0    0    0    0    0
4. Medeama    0    0    0    0    0    0    0

Ratiba:
Nov 25, 2023
CR Belouizdad v Yanga (ugenini)

Des 02, 2023
Yanga v Al Ahly (nyumbani)

Des 12, 2023
Medeama v Yanga (ugenini)

Des 19, 2023
Yanga v Medeama (nyumbani)

Des 24, 2023
Yanga v CR Belouizdad

Mar 02, 2024
Al Ahly v Yanga

        P    W    D    L    F    A    PTS
1. Wydad CA    0    0    0    0    0    0    0
2. Simba        0    0    0    0    0    0    0
3. Asec Mimosas    0    0    0    0    0    0    0
4. Jwaneg Galaxy    0    0    0    0    0    0    0

Ratiba:
Nov 25, 2023
Simba v Asec Mimosas (nyumbani)

Des 02, 2023
Jwaneg Galaxy v Simba  (ugenini)

Des 09, 2023
Wydad v Simba (ugenini)

Des 19, 2023
Simba v Wydad (nyumbani)

Des 24, 2023
Asec Mimosas v Simba (ugenini)

Mar 02, 2024
Simba v Jwaneg Galaxy (nyumbani)