Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dar Youth Cup yaanza kwa kishindo Lugalo

DAR Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi juzi yameanza katika hatua ya makundi ambapo mechi mbili zilipigwa kwenye viwanja vya Lugalo, Ufundi jijini Dar es Salaam.

MASHINDANO ya vijana ya Dar Youth Cup U-18 yameanza kwa kishindo wikiendi iliyopita kufuatia mechi za ufunguzi zilizopigwa Oktoba 10 kwenye viwanja vya Ufundi, Lugalo ikiwa ni msimu wa saba mfululizo yanafanyika.

Mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi juzi yameanza katika hatua ya makundi ambapo mechi mbili zilipigwa kwenye viwanja vya Lugalo, Ufundi jijini Dar es Salaam.

Kiujumla yanajumuisha timu nane zilizo katika makundi mawili A na B, na mechi ya ufunguzi ilikuwa ni kati ya Spotlight dhidi ya West FA iliyoanza saa 8:00 mchana, ikamalizika kwa sare ya 0-0 licha ya kosakosa nyingi.

Mechi ya pili ilikuwa ni kati ya Kakakuona dhidi ya TDS iliyoanza saa 10:00 jioni ambayo ilimalizika kwa TDS kuibuka na furushi la mabao 9-1, huku mchezaji wa TDS, Abiud Richard Faru akifanikiwa kufunga hat-trick.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hizo za ufunguzi, kocha mkuu wa TDS, Henry Sempa amesema: “Nashukuru mechi yetu ya ufunguzi ilikuwa nzuri, tumepata matokeo lakini pia jambo zuri ni kwamba tumepata nafasi ya kuona kile tunachokifanyia kazi katika kiwanja cha mazoezi kikiwa kinafanyika katika mechi. Kwa kiasi kikubwa kilichotupa nafasi ya kupata matokeo haya ni uwezo wa kuweza kupora mipira katika nusu yao.”

“ Sisi tunaamini sana kwenye maendeleo ya wachezaji na hapo unazungumzia ni kuwapa nafasi ya kucheza mechi za kiushindani baada ya kufanya mazoezi. Wanapopata mashindano kama haya wanaongeza uzoefu zaidi na kukua, jambo linalowafanya wawe tegemeo zaidi,”ameongeza.

“Tumekuwa tukifanya scouting pia kuangalia wachezaji wanaoweza kuingia katika vikosi vyetu hususani katika mashindano kama haya, ili kuweza kusaidia taifa. Hivyo ni jambo muhimu sana kuendelea kuwa na mashindano kama haya ya Dar Youth Cup,” amesema.

Mbali na Kocha Mkuu wa TDS ambayo ni timu maalum iliyoanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania chini ya programu maalum ya utambuzi wa vipaji, kocha wa Kakakuona, Zana Litemba ambaye timu yake imeanza vibaya kwa kipigo hicho cha mabao 9-1, amesema wanashukuru na wanafuraha sana ya kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo kwa upande wa U-18, licha ya kutoanza vizuri.

“Hatujakata tamaa, bado kuna mechi kadhaa za kucheza. Sisi tunaenda kujipanga kwenye kiwanja cha mazoezi kuhakikisha haya makosa ya leo hayajirudii. Kama ulivyoona kulikuwa na makosa mengi sana kuanzia kwa kipa wetu na safu ya ulinzi kwa ujumla, lakini hii imeshapita, tunajipanga kwa ajili ya mechi ijayo.”

Vilevile mchezaji bora wa mechi ya pili kati ya TDS na Kakakuona, Richard Faru, amesema: “Leo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kucheza mashindano haya, lakini nashukuru kwa kufunga mabao matatu na kuibuka mchezaji bora. Mechi ilikuwa nzuri sana, licha ya idadi ya mabao tuliyofunga, wapinzani wetu walionyesha kiwango bora ingawa tulifanikiwa kuwazidi kimbinu. Binafsi najipanga kuelekea mechi zijazo ili niweze kufanya vizuri zaidi.”

Mashindano hayo yaliendelea jana, kwenye viwanja hivyo vya Lugalo ambapo zilipigwa mechi mbili za Kundi B. Mechi ya kwanza ilizikutanisha Magnet Youth Sports Academy dhidi ya New Life Soccer Academy kuanzia saa 8:00 mchana, wakati mechi ya pili ikiwa kati ya Bulls Football Academy dhidi ya Brothers Jr iliyoanza saa 10:00 jioni.