Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chirwa: Dar Youth League imetutoa usingizini makocha

DAR Pict

Muktasari:

  • Chirwa ambaye ni kocha wa Spotlight Academy alisema tangu mwanzo wa mashindano kiwango cha ushindani kilikuwa cha juu, huku akimpongeza mwanzilishi na mkurugenzi wa mashindano hayo, Fina Mango kwa kuwezesha vijana kupata jukwaa la kushindana.

KOCHA Bora Martin Stephan Chirwa wa mashindano ya Dar Youth League U-15 yaliyomalizika jana katika viwanja vya Gymkhana kwa Simba Youth U-15 kuchukua ubingwa mbele ya Bulls Football Academy amesema yamekuwa na ushindani mkubwa kuwapa makocha na wachezaji nafasi ya kujifunza, kuonyesha uwezo na kupima maendeleo.

Chirwa ambaye ni kocha wa Spotlight Academy alisema tangu mwanzo wa mashindano kiwango cha ushindani kilikuwa cha juu, huku akimpongeza mwanzilishi na mkurugenzi wa mashindano hayo, Fina Mango kwa kuwezesha vijana kupata jukwaa la kushindana.

“Ukweli, hii League ya Dar Youth League inachezwa ki-pro sana. Tangu mwanzo wa mechi mpaka siku ya mwisho, ubora ni wa hali ya juu,” alisema Chirwa.

Alisema michuano hiyo pia imekuwa muhimu kwa makocha kwa sababu imewapa nafasi ya kupima uwezo wa timu katika mazingira halisi ya ushindani na kuwatoa usingizini.

Dar Youth League U-15 mwaka huu ilifanyika kwa mfumo wa ligi, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia yake ya miaka saba.

Timu nane zilishiriki na kila moja kucheza mechi sita katika hatua ya ligi, kabla ya timu nne zilizofanya vizuri zaidi kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika hatua hiyo ya nusu, Simba U-15 iliifunga West Football Academy mabao 2-0, huku Bulls Football Academy ikiichapa Safari Football Academy mabao 4-0 na kutinga fainali.Kwa upande wa fainali  Simba U-15 ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Bulls Football Academy mabao 2-0.

Mbali na ushindani wa ubingwa, mashindano hayo yameendelea kuwa sehemu muhimu ya kuwapa vijana nafasi ya kuonekana na kupata fursa katika soka la ushindani.

Chirwa alisema hakutarajia kutambuliwa kwa namna hiyo, lakini tuzo hiyo imempa hamasa ya kuongeza juhudi katika kazi yake. “Kwangu leo imekuwa mshtuko kidogo, sikutarajia, ila zaidi ya yote jicho limeniona mimi. Nami sina budi kushukuru sana na kunifanya nizidishe juhudi,”   alisema.

Chirwa alisema tuzo hiyo ni motisha kwake kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kukuza vipaji vya vijana.

Mwanzilishi na mkurugenzi wa Dar Youth League, Fina Mango alisema wana mpango wa kupanua mashindano hayo na kuyafikisha katika maeneo mengine nchini, ingawa hatua hiyo inahitaji maandalizi.

Mashindano hayo yamefanyika kwa msimu wa saba, huku mfumo wa ligi ukiendelea kwa msimu wa pili yakiwa ni mabadiliko mapya yaliyolenga kuongeza ushindani na kuwapa vijana michezo ya kutosha.

Msimu huu pia Dar Youth League imepata sapoti kutoka kampuni ya Howden Puri, huku mkurugenzi mtendaji wake, Umesh Puri, akisema wamefurahishwa kuunga mkono mpango unaotumia michezo kuwaandaa vijana. wakijivunia kushirikiana na mipango inayowapa fursa.