Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamtuwezi; JB, wenzake walivyoitambia Yanga, Nature adai haijaisha

WASANII Pict

Muktasari:

  • Baada ya Dabi ya Kariakoo iliyopigwa juzi Jumamosi, Oktoba 10, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga, wasanii wanaozishabikia timu hizo wamepata sababu nyingine ya kutambiana, huku kila upande ukiwa na namna yake ya kupokea matokeo hayo.

USHINDANI wa Simba na Yanga hauishii kwenye dakika 90 za mechi pekee, bali huendelea pia kwenye midomo ya mashabiki, wakiwemo wasanii wanaozitumia timu hizo kama sehemu ya burudani yao.

Baada ya Dabi ya Kariakoo iliyopigwa juzi Jumamosi, Oktoba 10, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga, wasanii wanaozishabikia timu hizo wamepata sababu nyingine ya kutambiana, huku kila upande ukiwa na namna yake ya kupokea matokeo hayo.

Miongoni mwa wasanii wanaoshabikia Simba ni Inspector Haroun, JB, Amini na Whozu, huku upande wa Yanga ukiwakilishwa na Mzee Yusuf, Juma Nature, Kusah na Chaz Baba wamezungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti wamesema haya baada ya Dabi:


WASA 08
WASA 08

Inspector Haroun

Inspector Haroun, maarufu Babu, ametamba baada ya Simba kuichapa Yanga mabao 2-1, amesema matokeo hayo yametimiza utabiri wake wa kabla ya mchezo Mnyama angeshinda kwa mabao mawili.

“Hatutaki kelele, roho zimetulia sasa, na utabiri wangu umetumia, ila Rushine apewe mapumziko, kiwango kinashuka. Jana ameshindwa kucheza jihadi. Kwenye bao la Cassali, Derick alitakiwa kuzuia, lakini alionekana kuchelewa. Mwalimu awape nafasi mabeki wengine, Rushine apumzike atarudi vizuri, lakini dirisha dogo tupate kipa,” amesema Babu.


WASA 01

JB

Muigizaji JB naye anaingia kwenye orodha ya mashabiki wa Simba wenye sababu ya kufurahia matokeo hayo.

Amesema ni zamu yao Simba kucheka kwani ushindi wa timu yake unampa nafasi ya kuwatania mashabiki wa Yanga, ambao safari hii wamejikuta upande wa wapotezaji.

“Leo ni siku ya Simba kufurahia ushindi, Yanga wasubiri nafasi nyingine ya kulipa kisasi ila kwa sasa watuache kidogo.”


WASA 02

Amini

Kwa Amini, ambaye amekuwa akionyesha mapenzi yake kwa Simba, ushindi wa mabao 2-1 kwake ni nafasi ya kusisitiza mshikamano wa mashabiki wa timu, Viongozi Pamoja na wachezaji ndicho kilichowamaliza Yanga.

“Simba Nguvu Moja ndiyo imesababisha Yanga kupata kipigo cha dabi hii, tumemtafuta sana furaha hii kwa muda sasa. Leo hii Yanga hawana cha kuniambia sababu mpira uliochezwa pale uwanjani hata wao hawakuwahi kucheza vile Pamoja na walitufunga mechi za nyuma.”


WASA 03

Whozu

Msanii wa Bongo Fleva Whozu naye anaingia kwenye upande wa washindi. Kwa mashabiki wa Simba, ushindi dhidi ya Yanga  anasema ni matokeo yenye ladha ya pekee kwa sababu ushindani wa timu hizo huambatana na utani wa muda mrefu.

“Nasemaje safari hii Mnyama ndiye aliyewazidi kete Yanga, sasa hapa waendelee kusubiri dabi inayofuata kupigwa tena yaani hapa gari ndio lishawaka kulizima yanga watasubiri sana.”


WASA 04

Mzee Yusuf

Mzee Yusuf ni miongoni mwa shabiki wa Yanga, nasema haikuwa bora sana yanga ila anataka Simba irudishe yale mabao waliyofungwa na Yanga.

“Mimi nawakumbusha Simba ushindi wa mchezo mmoja hauondoi ushindani wa muda mrefu kati ya timu hizo mbili. Sawa yanga haikuwa bora sana  lakini Simba wanatakiwa warudishe zile goli zote walizofungwa kwenye mechi zote.”


WASA 05

Juma Nature

Kachukizwa na kichapo na kafunguka simba wajipange watalipa kisasi; “Sawa wameshinda, ila Simba wasione kama wamemaliza, bado kuna michezo mingine mbele yao na tutakuja tu kukutana nao tena na tutawapiga tu.”


WASA 06

Kusah

“Nimepokea matokeo ya dabi vibaya  sema  safari hii Simba imepata ushindi, lakini siyo kuwa wamepaga ubingwa, niwaombe tu mashabiki wenzangu wa yanga waendelee kuiunga mkono timu yao licha ya matokeo hayo.”


WASA 07

Chaz Baba

“Tutarudi kwa nguvu zote, matokeo haya hayawezi kuturudisha nyuma, kikubwa wachezaji na viongozi waangalie mbele na kusubiri nafasi nyingine ya kuonyesha ubora wa timu yetu

Katika ushindani wa Simba na Yanga, kupoteza mchezo mmoja hakumalizi utani.”

Mashabiki wa timu ya Simba  huendelea kujivunia matokeo, huku Yanga wakisubiri nafasi ya kujibu kwenye dabi inayofuata.


Dakika 90 zimekwisha, utani unaendelea

Ushindi wa Simba wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga umeongeza ukurasa mwingine katika historia ya ushindani wa timu hizo kongwe nchini.

Kwa wasanii wanaozishabikia timu hizo, matokeo hayo yanatoa nafasi ya kuendeleza utani unaochanganya soka na burudani.

Hata hivyo, ushindani huo hauishii kwa wasanii pekee, kwani mashabiki wa timu hizo huendelea kutambiana kwenye mitandao ya kijamii, sehemu za kazi na hata ndani ya familia.