Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dar yapata sababu mpya ya mtoko Alhamisi

KIPYA Pict

KWA miaka mingi, Ijumaa imekuwa siku rasmi ya kuanza burudani za mwisho wa wiki jijini Dar es Salaam lakini kwa sasa, Kalito’s Way Group (KWG) imeamua kubadili mtindo huo kwa kuwapa wakazi wa jiji hilo sababu za mtoko siku moja kabla katika matawi yake yote matatu.

Wazo hilo limetokana na  uhalisia wa maisha ya kila siku baada ya wiki nzima ya kazi, wapo wanaotaka kupumzika, kukutana na marafiki na kubadili mazingira kabla ya kurejea kwenye majukumu ya siku inayofuata. Kwa KWG, Alhamisi inaweza kuwa zaidi ya siku ya kawaida katikati ya wiki, bali mwanzo wa burudani za mwisho wa wiki.

Dhana hiyo ilizinduliwa Oktoba 8, 2026, katika matawi matatu ya kundi hilo, Wavuvi Kempu, Samaki Samaki na Kuku Kuku. Uzinduzi huo ulihusisha rangi za kuvutia, mapambo maalumu na wahusika waliovalia mavazi yaliyochota msukumo kutoka Japan huku kila eneo likiwa na mtindo wake wa burudani. Badala ya kurudia tukio moja katika maeneo yote, KWG iliandaa dhana tatu tofauti zilizolenga kumpa mteja sababu ya kuchagua mazingira yanayomfaa.

KIPY 01

Katika Wavuvi Kempu, rangi ya zambarau ndiyo iliyotawala kupitia Purple Thursdays. Taa, mwonekano wa eneo na mavazi ya DJ viliendana na dhana hiyo na kuifanya rangi hiyo kuwa sehemu ya utambulisho wa burudani za Alhamisi.

“Tuliamua kubadilisha Alhamisi ya Wavuvi, ndiyo maana tukaipa Purple Thursday,” alisema Lauren Kamshange, meneja wa KWG. Wazo ni kuifanya kila eneo iwe na ladha yake huku mazingira yakisaidia kutofautisha burudani hiyo na matukio mengine ya kawaida.

KIPY 02

Samaki Samaki nayo imekuja na Toroka Uje, dhana inayolenga kuwavutia watu mara tu wanapomaliza kazi. Inayoanza saa 4:00 usiku, kampeni hiyo imeambatana na mabadiliko ya mwonekano wa eneo na maandalizi maalumu yanayolenga kuipa Alhamisi sura tofauti.

“Tunataka watu wanapotoka kazini wasiende moja kwa moja nyumbani. Wanaweza kuja Samaki Samaki na kufurahia kama ilivyo Ijumaa, kama mwisho wa wiki,” alisema Kamshange. Hapo ndipo jina Toroka Uje linapopata maana yake ya burudani kutoka kwenye pilikapilika za siku na kuingia katika mazingira tofauti ya kujipumzisha.

KIPY 03

Kuku Kuku imechagua njia tofauti zaidi kupitia Tokyo Thursdays, dhana iliyochota msukumo kutoka Japan na taswira zinazohusishwa na wahusika wa ninja. Mavazi ya wahusika, mapambo na mazingira yaliyobadilishwa vinalenga kumpa mteja hisia ya kuingia kwenye ulimwengu mwingine bila kuondoka jijini Dar es Salaam.

“Watu wanapofika huko, wanakutana na mazingira tofauti. Hili halijawahi kutokea hapa Tanzania, na tunaamini hata Afrika au duniani kote. Kwa hiyo tunawapa watu uzoefu mpya,” alisema Kamshange.

KIPY 03 (1)

Hata hivyo, nguvu ya Kionjo Chetu haipo tu kwenye dhana hizo tatu, bali pia namna zilivyounganishwa kupitia Route 360. Mpango huo unawawezesha wateja kutembelea matawi mbalimbali ya kundi hilo na kupata uzoefu tofauti ndani ya safari moja ya burudani.

KIPY 05

Mteja anaweza kuchagua mazingira ya zambarau Wavuvi Kempu, kuendelea na Toroka Uje Samaki Samaki au kuelekea Kuku Kuku kwa ajili ya Tokyo Thursdays, kulingana na aina ya burudani anayoipendelea.