Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika tisa za Mtasingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns

MTWASINGWA Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa FNB, Johannesburg kati ya Kaizer dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini huku dakika 90 zikimalizika kwa sare ya 1-1.

KIUNGO Mtanzania, Adolf Mtasingwa ameendelea kupata nafasi kwenye kikosi cha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya Agosti 15 kucheza kwa dakika tisa akiingia kutokea benchi.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa FNB, Johannesburg kati ya Kaizer dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini huku dakika 90 zikimalizika kwa sare ya 1-1.

Mtasingwa aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Lebohang Maboe dakika ya 82, wakati Kaizer Chiefs ikiwa tayari imeruhusu bao lililowekwa kambani na Cassius Mailula dakika ya 75 na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kwenye mechi hiyo ambayo Kaizer ilikuwa inaongoza Mtasingwa alionyesha kiwango bora, utulivu kwenye eneo la kati na kutuliza tempo ya mchezo.

Kiungo huyo ambaye alijiunga na kikosi cha Amakhosi akitokea Azam FC imekuwa muendelezo kwake kupewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kocha Fernando Da Cruz.

Mechi yake ya kwanza kucheza ilikuwa Julai 27 alipoanza kwenye mechi ya Kombe la Toyota Cup ambapo kikosi hicho kilinyakua taji hilo lililokuwa linatetewa na Yanga iliyobeba msimu uliopita.

Licha ya kwamba ni mgeni kwenye ligi hiyo lakini Mtasingwa kila anapopata nafasi ya kucheza ameonyesha kiwango bora kiasi cha kumshawisho kocha huyo kuendelea kumtumia.