Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika 90 nzito AFCON U-23

AFCON Pict

Muktasari:

  • Tanzania inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kibarua kizito cha kupindua matokeo ya kichapo cha mabao 4-1 ilichokipata Septemba 28, 2026 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

LEO saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Timu ya Taifa ya U-23 itakuwa na dakika 90 ngumu dhidi ya Kenya kwenye mechi ya marudiano kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana mwakani Misri.

Tanzania inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kibarua kizito cha kupindua matokeo ya kichapo cha mabao 4-1 ilichokipata Septemba 28, 2026 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Ili kufufua matumaini na kusonga mbele katika hatua inayofuata ambapo mshindi wa jumla atakutana na Ivory Coast, Tanzania inahitaji kupata ushindi wa mabao 3-0.

ACF 01

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Shekhan Khamis amesema wachezaji wamejiandaa vizuri na wanafahamu ugumu watakaokutana nao kwenye mechi hiyo muhimu nyumbani.

“Tunafahamu hatukucheza vizuri ugenini lakini tuko nyumbani na tunayo nafasi ya kushinda kama tutafuata maagizo ya kocha na tunaamini tunayo nafasi ya kufanya vizuri ingawa sio rahisi,” amesema Shekhan.

Kocha wa Tanzania, Ahmad Ally alipozungumza na gazeti hili amesema ingawa kuna baadhi ya majeruhi lakini wanaamini wachezaji watafanya vizuri na kuhakikisha wanafuzu hatua ya pili.

ACF 02

“Mabeki wetu wawili wote waliumia na hawapo kwenye mpango wa mechi hivyo tumewaongeza wachezaji wengine Abubakar Nizar ‘Ninju’ na  Evastus Lukanimi waliokuwa timu ya taifa ya U-20 pia Issa Abushiri ambaye tulimuongeza daktari aligundua ana kidonda mguuni hivyo hatakuwepo,” amesema Ahmad na kuongeza:

“Nafikiri ugumu wa mechi upo kwenye idadi hiyo ya mabao tunayopaswa kuyafunga lakini kwa jinsi tulivyocheza tayari kila timu inafahamu ubora na udhaifu wa mwenzie.”

Tanzania ambayo hii ni mara yao ya tano kushiriki mashindano hayo ya kufuzu AFCON inatafuta historia ya kucheza fainali hizo ambazo mara zote ilizoshiriki tangu mwaka 2011 yalipoanzishwa mashindano hayo haijawahi kufuzu.