Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Daddy aibeba Chipukizi Ligi Kuu Zanzibar

DADY Pict

Muktasari:

  • Dady alianza kwa kufunga bao dakika ya 11, kisha kutoa asisti iliyotumiwa na Mwadini Ali kufunga bao la pili dakika ya 15, na kuifanya Chipukizi kuondoka na ushindi huo katika Ligi Kuu Zanzibar, mchezo uliochezwa Novemba 18, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

KIUNGO mshambuliaji wa Chipukizi United, Dady Francis ameendeleza mchango wake katika kikosi hicho baada ya kuhusika moja kwa moja katika mabao mawili yaliyoipa timu hiyo ushindi wa 2-1 dhidi ya KMKM SC.

Dady alianza kwa kufunga bao dakika ya 11, kisha kutoa asisti iliyotumiwa na Mwadini Ali kufunga bao la pili dakika ya 15, na kuifanya Chipukizi kuondoka na ushindi huo katika Ligi Kuu Zanzibar, mchezo uliochezwa Novemba 18, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo huyo amesema Chipukizi ilitumia mfumo wa kujilinda kwa umakini huku ikitumia kasi kushambulia kila ilipopata nafasi.

Amesema timu hiyo imeimarika kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu, jambo linalowapa matumaini ya kuendelea kupata matokeo mazuri katika michezo ijayo.

“Najisikia vizuri kuhusika katika mabao mawili tuliyofunga. Jambo hilo limeongeza hamasa kwangu na kunipa nguvu ya kuendelea kufunga ili nipate timu katika dirisha dogo la usajili,” amesema Dady.

Alifafanua kuwa kilichomfurahisha zaidi ni kufunga bao kwa kichwa, akitumia vizuri asisti ya Juma Khatib aliyetengeneza nafasi hiyo kupitia mpira wa adhabu.

Mbali na kueleza furaha yake kwa mchango alioutoa katika ushindi huo, Dady aliwapongeza mashabiki wa Chipukizi kwa kuendelea kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kujituma ili kutowaangusha.