Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara Luvanga azidi kutikisa kimataifa

Muktasari:

  • Luvanga alifunga mabao hayo katika mchezo wa hatua ya awali ya mashindano hayo, uliochezwa juzi Jumapili huku Al-Nassr ikimaliza hatua hiyo kwa ushindik mubwa.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga, ameendelea kuiweka bendera ya Tanzania juu katika soka la kimataifa, baada ya kufunga mabao saba katika ushindi wa mabao 12-0 wa Al-Nassr dhidi ya CSKA Dushanbe ya Tajikistan, katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia.


Luvanga alifunga mabao hayo katika mchezo wa hatua ya awali ya mashindano hayo, uliochezwa juzi Jumapili huku Al-Nassr ikimaliza hatua hiyo kwa ushindik mubwa.


Luvanga alianza kufungua akaunti ya mabao katika dakika ya 33, kisha kuongeza mengine katika dakika ya 35 na 39 na kuifanya Al-Nassr kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 6-0.


Baada ya mapumziko, mshambuliaji huyo wa Kitanzania aliendelea na kasi yake kwa kufunga mabao katika dakika ya 69 na 74, kisha kupachika mengine katika dakika za 87 na 89.

Mabao mengine ya Al Nassr katika mechi hiyo yalifungwa na Hessa Al Isa aliyefunga matatu na Rinas Saleh na Basmah Al Shnaifi waliopachika bao moja kila mmoja, kukamilisha ushindi huo mkubwa na wa kihistoria.


Hata hivyo, licha ya ushindi huo mnono,safari  ya Al Nassr iliishia hapo kwani haikufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia.


Kabla ya mchezo huo, Al-Nassr ilikuwa imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Bam Khatoon ya Iran.


Katika mchezo huo, Luvanga ndiye aliyefunga bao la Al-Nassr kwa mkwaju wa penalti dakika ya 84, lakini Sara Didar aliisawazishia Bam Khatoon katika dakika ya nyongeza na kuipa timu hiyo ya Iran nafasi nzuri ya kuongoza kundi.


Bam Khatoon baadaye ilimaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi E, ikiwa na pointi saba na kupata tiketi ya kufuzu hatua ya makundi, wakati Al Nassr katika ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi tano.

CSKA Dushanbe ilimaliza bila pointi baada ya kupoteza mechi zake zote tatu.


Luvanga ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga Princess anazidi kuandika historia nyingine katika safari yake ya soka la kimataifa.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, ameichezea Al Nassr katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia kwa misimu kadhaa na amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa klabu hiyo.


Takwimu zinaonyesha kuwa, katika msimu wa 2026/27 wa mashindano hayo, amefanikiwa kufunga mabao tisa kwenye michezo mitatu.


Mwaka 2024, akiwa na umri wa miaka 19, alifunga mabao mawili katika ushindi wa Al-Nassr wa mabao 3-0 dhidi ya Yadroan, katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia.


Takwimu zake za jumla tangu ajiunge na Al Nassr ni msimu wa 2023/24 alifanikiwa kufunga mabao 11 na kutengeneza nafasi nane za usaidizi.

Msimu wa 2024/25, alifanikiwa kufunga mabao 19 na kutengeneza nafasi saba zilizotumiwa na wachezaji wenzake kufunga mabao, wakati msimu wa 2025/26, alifanikiwa kupachika mabao 24 na kutengeneza nafasi tatu.


Hii ina maana kwamba, nyota huyo amefanikiwa kufunga mabao 54 na kutengeneza nafasi 18,tangu alipojiunga na Al Nassr.


Mafanikio yake yanaendelea kuongeza mwanga kwa soka la wanawake nchini, huku Luvanga akiwa mmoja wa wachezaji wa Kitanzania wanaocheza nje ya nchi na kuendelea kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.


Tukirejea hapa nchini, msimu wa 2022/23,Clara akiwa na kikosi cha Yanga Princess alifanikiwa kufunga mabao 13.


Akicheza kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17(Serengeti Girls)alifanikiwa kufunga mabao 10 katika michezo sita akiyokuwa dimbani.


Mchango wake unakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha Tanzania kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 zilizofanyika nchini India mwaka 2022.