Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madogo janja EPL walioanza na ukali

MADOGO Pict

Muktasari:

  • Hawa hapa ni mastaa 10 wapya wenye umri wa kati ya miaka 18 na 21 ambao katika miezi michache ijayo ambao wanastahili kuangaliwa kwa karibu, kwani wanaweza kuushangaza ulimwengu wa mashabiki wa soka duniani baada ya kutua katika ligi hiyo msimu huu.

LONDON, ENGLAND: IKIWA tayari imesharejea kwa ajili ya msimu wa 2026/27, Ligi Kuu England imeshuhudiwa raundi ya kwanza ikimalizika jana, huku sura mpya zikianza kuchomoza na kuvuta hisia za mashabiki wa soka.

Hawa hapa ni mastaa 10 wapya wenye umri wa kati ya miaka 18 na 21 ambao katika miezi michache ijayo ambao wanastahili kuangaliwa kwa karibu, kwani wanaweza kuushangaza ulimwengu wa mashabiki wa soka duniani baada ya kutua katika ligi hiyo msimu huu.

MADO 01

Bazoumana Toure (Newcastle United)

Anthony Gordon ameacha nafasi kubwa ya kujazwa Newcastle United, lakini Bazoumana Toure mwenye umri wa miaka 20 ana uwezo wake ambao unaweza kumfanya kuwa mbadala mzuri. Hata hivyo, siyo mchezaji anayefanana kabisa na Gordon.

Toure ana kasi kubwa na ni winga wa kizamani zaidi, akicheza zaidi upande wa kushoto na akiwa mguu wake wa kushoto ndio wenye nguvu. Kutokana na hilo, alikuwa mtengeneza nafasi zaidi kuliko mfungaji alipokuwa Hoffenheim msimu uliopita.

Katika michango yake 14 ya mabao kwenye Bundesliga msimu uliopita, alitoa pasi tisa za mabao. Pia alitengeneza nafasi 44 katika mchezo wa wazi, idadi iliyozidiwa na wachezaji watano pekee. Alipiga mashuti 48, idadi inayokaribiana na Gordon. Lakini, Gordon alitengeneza nafasi 24 pekee katika mchezo wa wazi akiwa Ligi Kuu England msimu uliopita, huku naye akipiga mashuti 48.

Toure pia ni mchezaji anayependa kupiga krosi nyingi. Alipiga krosi 115 katika mchezo wa wazi, ikiwa ni idadi ya nne kwa wingi zaidi Bundesliga msimu uliopita. Kwa hiyo, atakuwa tofauti na Gordon, lakini anaweza kuwa chanzo muhimu cha hatari kwa Newcastle.

MADO 02

Christos Tzolis (Arsenal)

Ingawa Leandro Trossard huenda asiwe jina kubwa zaidi katika Ligi Kuu England, alikuwa mchezaji muhimu na anayeaminika Arsenal. Kwa hiyo, kumtafutia mbadala siyo jambo rahisi.

Christos Tzolis ndiye aliyepewa jukumu hilo, na kwa mtazamo wa mwanzo anaonekana kuwa mchezaji anayefaa kwa kazi hiyo.

Kwanza, alikuwa mtengeneza nafasi mwenye ufanisi mkubwa akiwa Club Brugge msimu uliopita, akitengeneza 135, ikiwa ni 35 zaidi ya mchezaji mwingine yeyote katika Ligi Kuu Ubelgiji. Jambo muhimu zaidi kwa Arsenal ni uwezo wake katika mipira iliyokufa, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa mipira ya adhabu na kona kwa The Gunners.

Mchezaji wa Arsenal aliyekuwa ametengeneza nafasi nyingi zaidi kutokana na mipira iliyokufa msimu uliopita alikuwa Declan Rice (27). Tzolis alitengeneza nafasi 52 kutokana na mipira hiyo. Hiyo ilikuwa asilimia 38.5 ya nafasi zake zote alizotengeneza. Rice alikuwa na uwiano bora zaidi, asilimia 42.9, lakini jumla ya nafasi 63 ilikuwa ndogo zaidi ukilinganisha na Tzolis.

Haitegemewi Tzolis kufikia kiwango cha michango 40 ya mabao aliyokuwa nayo msimu uliopita, lakini itakuwa jambo la kuvutia kuona jinsi atakavyozoea ligi hiyo. Tayari alishatoa ishara nzuri katika ushindi wa Arsenal dhidi ya Manchester City kwenye Ngao ya Jamii alipotoa asisti mbili.

MADO 03

Mamadou Sangare (Brentford)

Kuna wataalamu wengi wa soka la Ufaransa walioshangazwa kuona Mamadou Sangare akiishia kujiunga na Brentford msimu huu. Ukweli kwamba raia huyo wa Mali alikuwa na msimu mmoja tu wa uzoefu katika ligi kubwa huenda ulizifanya baadhi ya timu kusita kumsajili.

Brentford, hata hivyo, inaonekana kufaidika kutokana na kusita kwa wengine. Sangare alidhihirisha kuwa kiungo mwenye uwezo mkubwa akiwa Lens msimu wa 2025/26. Katika ligi tano bora za Ulaya msimu uliopita, ni Elliot Anderson na Exequiel Palacios pekee waliokuwa na wastani bora wa kurejesha umiliki wa mpira kwa kila dakika 90 kuliko Sangare aliyekuwa na wastani wa 8.01 kwa kila dakika 90. Alipocheza eneo la kati la uwanja alirejesha mpira mara 4.7 kwa kila dakika 90, ikiwa ni nafasi ya pili kwa ubora.

Lakini, Sangare pia alikuwa na mchango mkubwa akiwa na mpira. Ni wachezaji wanne tu wa Ligue 1 waliotengeneza nafasi za pili zaidi kuliko 31 alizotengeneza. Pia, kwa kila dakika 90, viungo wanne pekee walikuwa na wastani bora kuliko ushiriki wake wa 6.3 katika mfululizo wa mashambulizi yaliyomalizika kwa shuti. Anatumia mpira kwa akili na ni mchezaji anayeaminika katika ujenzi wa mashambulizi, kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi na kuhifadhi mpira akiwa chini ya presha.

MADO 04

Zadok Yohanna (Brighton)

Huenda akahitaji muda na uvumilivu, na bado ana mambo mengi ya kujifunza, lakini ikiwa Zadok Yohanna atapata nafasi Brighton msimu huu bila shaka atavutia macho ya mashabiki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kutoka Nigeria alijiunga na Brighton akitokea AIK kwa ada iliyoripotiwa kuwa Pauni 21.5 milioni, ikiwa ni rekodi ya mauzo katika soka la Sweden, licha ya kucheza mechi 13 pekee. Hilo lilitosha kuishawishi Brighton, ambayo inaonekana kuvutiwa na mtindo na ujasiri wake wa kuwachambua wapinzani kwa chenga.

Yohanna ni winga wa kulia anayetumia mguu wa kushoto. Kabla ya uhamisho wake kuthibitishwa alikuwa na wastani wa majaribio 8.5 ya chenga kwa kila dakika 90 alipokuwa Allsvenskan, zaidi ya mchezaji mwingine yeyote katika ligi hiyo.

Katika kipindi hicho, pia alikuwa kinara kwa kuingia kwenye boksi kwa chenga mara sita, kuwapita wapinzani ndani ya boksi mara 15, na alikuwa miongoni mwa waliokuwa na idadi kubwa zaidi ya chenga zilizofuatiwa na shuti, akiwa na tatu, licha ya kucheza dakika chache zaidi kuliko wachezaji wengi. Bado anahitaji kuboresha umaliziaji wake, lakini ana uwezo wa kuwainua mashabiki kutoka kwenye viti.

MADO 05

Hay den Hackney (Everton)

Ha yden Hack ney alijijengea sifa kubwa katika misimu yake minne Championship akiwa Middlesbrough, baada ya kupitia akademi ya klabu hiyo. Lakini, baada ya Boro kushindwa kupanda daraja msimu uliopita, ilionekana kuwa vigumu kwa mchezaji huyo wa zamani wa timu ya England chini ya miaka 21 kubaki. Everton ndiyo iliyofanya uamuzi wa kumsajili kwa ada iliyoripotiwa kuwa Pauni 16.5 milioni.

Hackney ni kiungo mwenye usahihi katika kumiliki mpira, lakini pia ana uwezo wa kusogeza mchezo mbele kupitia pasi. Asilimia 33.5 ya pasi zake za mchezo wa wazi alizopiga zilikuwa za mbele, kiwango kilichokuwa karibu na wastani wa wachezaji wa nafasi yake katika Championship msimu uliopita. Hata hivyo, alitengeneza nafasi za pili 52, ambazo zilikuwa nyingi zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote katika ligi hiyo.

MADO 06

Emersonn (Ipswich Town)

Mara ya mwisho Ipswich ilipocheza Ligi Kuu England msimu wa 2024/25 iliamini katika mshambuliaji Liam Delap. Safari hii imefanya hivyo tena baada ya kutumia Pauni 24 milioni zilizoripotiwa kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Emersonn, kutoka Toulouse.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ni aina fulani ya kamari. Hajasajiliwa kutokana na msimu wenye mabao mengi, kwani alifunga sita pekee katika mechi 28 za Ligue 1 msimu uliopita. Hata hivyo, bado ana mambo mengi ya kutoa. Ana kasi, ni mrefu, ana uwezo mzuri wa kiufundi na ni mzuri katika kukimbia nyuma ya mabeki pamoja na kushuka chini kusaidia kuunganisha timu.

Msimu uliopita alikuwa wa nane kati ya washambuliaji wa kati wa Ligue 1 kwa idadi ya kukokota mpira ulioishia kuwa shuti au kutengeneza nafasi, akiwa na 17. Wengi wa waliokuwa mbele yake walicheza dakika nyingi zaidi. Itakuwa jambo la kuvutia kuona jinsi atakavyozoea ligi hiyo.

MADO 07

Johan Manzambi (Aston Villa)

Aston Villa imewapoteza Morgan Rogers na Youri Tielemans msimu huu, hivyo ilikuwa muhimu kupata nguvu zaidi ya kushambulia kutoka eneo la kiungo. Matumaini ni kwamba Johan Manzambi atasaidia kuziba pengo lililoachwa na wachezaji hao.

Manzambi, mwenye umri wa miaka 20, ni kiungo anayependa kusogeza mchezo mbele na mwenye uwezo wa kupenya kwenda mbele kwa kasi huku akiwakwepa wapinzani katika maeneo yenye msongamano. Akiwa Freiburg msimu uliopita, ni viungo watatu pekee Bundesliga waliokuwa na wastani bora kuliko Manzambi wa kukokota mpira mbele kwa angalau mita 10, akiwa na wastani wa 5.0 kwa kila dakika 90.

Pia, alikuwa wa 14 kwa majaribio ya chenga akiwa na 2.8 kwa dakika 90, huku wengi waliokuwa mbele yake wakiwa wachezaji wanaocheza zaidi kama mawinga. Baadaye alifanya vizuri katika Kombe la Dunia akiwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika kipindi cha angalau miaka 60 kufikisha michango mitano ya mabao katika shindano moja ikiwa ni mabao matatu na asisti mbili.

Manzambi alikuwa akiwindwa na klabu kadhaa katika vita vya uhamisho, lakini Aston Villa ilifanikiwa kumsajili. Uwezekano wa kuendelea kukua chini ya kocha Unai Emery unavutia.

MADO 08

Caleb Yirenkyi (Coventry City)

Coventry City ilipata sifa nyingi na pia iliwafanya wengine waionee wivu ilipotangaza kumsajili Caleb Yirenkyi kutoka Nordsjaelland ya Denmark mapema mwezi huu. Yirenkyi ni raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 20 ambaye alicheza Kombe la Dunia 2026. Hata hivyo, wataalamu wa takwimu walikuwa wakimfuatilia kwa muda kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali.

Kwa kawaida ni kiungo wa kati, lakini anaweza kucheza kama kiungo mkabaji, kati au hata beki wa kulia. Uwezo wake unaashiria kwamba anaweza kuwa mchezaji anayefaa Ligi Kuu England.

Katika Ligi Kuu Dermark msimu uliopita, alikuwa mmoja wa viungo sita pekee waliokuwa na wastani wa angalau nafasi moja iliyotengenezwa katika mchezo wa wazi, takolingi 1.5 na kurejesha umiliki wa mpira mara sita kwa kila dakika 90.

Kati ya hao, Yirenkyi alikuwa na mguso wa mpira 81.1 kwa dakika 90, ambao ulikuwa mkubwa kwa kiasi kikubwa, huku asilimia 91.8 ya pasi zake zikimfanya awe bora zaidi kati ya viungo wote katika mashindano hayo waliocheza angalau dakika 900.

Yirenkyi alikuwa juu ya wastani katika karibu kila kipengele, jambo ambalo linaonyesha uwezo wake mkubwa.

MADO 09

Lucas Herrington (Hull City)

Alicheza mechi yake ya kwanza Colorado Rapids mwezi Februari pekee, lakini Lucas Herrington aliitwa katika kikosi cha MLS All-Star baada ya kucheza Kombe lake la kwanza la Dunia akiwa na Australia. Kupanda kwake kumekuwa kwa kasi, hasa ikizingatiwa kwamba bado ana umri wa miaka 18. Alivutiwa na klabu kadhaa kubwa, lakini akaamua kujiunga na Hull City kwa sababu aliamini angepata nafasi nzuri zaidi ya kucheza kikosi cha kwanza, na juzi alikuwa uwanjani katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United.

Mchezaji huyo ni beki wa kati mwenye ustadi wa kucheza mpira kuanzia nyuma na ni miongoni mwa mabeki waliocheza zaidi ya dakika 400  MLS mwaka huu. Herrington alikuwa wa sita kwa mguso wa mpira kwa dakika 90 akiwa na 92.3, wa nane kwa usahihi wa pasi kwa asilimia 93.8, wa nne kukokota mpira kwa dakika 90 akiwa na 24.4, na wa tatu kwa kutoa pasi kwa zaidi ya mita 10 akiwa na 5.4 kwa dakika 90.

Huenda akahitaji muda kuzoea ugumu wa Ligi Kuu England, lakini kiwango chake cha kushinda mipira ya juu cha asilimia 71.2 katika MLS kilikuwa kizuri na kilimuweka nafasi ya 15 katika kundi la mabeki.

MADO 10

Tarik Muharemovic (Leeds United)

Leeds imemfanya Tarik Muharemovic kuwa mchezaji wake wa pili kwa thamani kubwa baada ya kulipa Sassuolo ada iliyoripotiwa kuwa Pauni 34 milioni mapema msimu huu. Anaonekana kuwa aina ya mabeki wa kati ambaye mashabiki watampenda haraka. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Bosnia na Herzegovina ana uwezo wa kiufundi katika safu ya ulinzi, pia ni beki mwenye nguvu na anayependa ushindani.

Muharemovic haogopi kucheza pasi za hatari. Pasi zake 191 ndefu zilikuwa za 11 kwa wingi zaidi kati ya wachezaji wote wa uwanjani katika Serie A msimu uliopita, huku akiwa kwa pamoja katika nafasi ya sita kubadilisha mwelekeo wa mchezo akifanya hivyo mara 12.

Katika mipambano ya kimwili alikuwa na kiwango cha mafanikio cha asilimia 69.8, ikiwa ni rekodi ya 10 kwa ubora katika Serie A msimu uliopita kati ya wachezaji waliokuwa na angalau takolingi 50.