Clara ajumuishwa kikosi cha Al Nassr

WIKI iliyopita Mwanaspoti liliandika kuwa straika wa zamani wa Yanga, Clara Luvanga atajuinga na Al Nassr ya Saudia.

Nyota huyo wa kimataifa kutoka Tanzania tayari amejiunga na timu hiyo na amepostiwa akijumuishwa kikosi cha msimu wa 2023/2024.

Ikumbukwe mchezaji huyo alikuwa akikipiga Dux Lugrono ya Hispania ambapo alidumu ndani ya miezi miwili.

Hivyo Clara atakuwa pamoja na Enekia Kasongo aliyejiunga na Eastern Flames ya nchini humo.