Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chirwa arejea Geita Gold

CHIRWA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2, Chirwa alifunga penalti dakika ya 45+8 na kushindwa kuendelea baada ya jeraha hilo.

MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, Mzambia Obrey Chirwa ameanza mazoezi na kikosi baada ya kupona jeraha la bega lililotokana na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC iliyopigwa Uwanja wa Bukombe, Geita, Agosti 28, 2026.

Katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2, Chirwa alifunga penalti dakika ya 45+8 na kushindwa kuendelea baada ya jeraha hilo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zubery Katwila amesema mshambuliaji huyo ameanza rasmi mazoezi na wachezaji wenzake na yupo fiti kucheza, jambo linalompa wigo mpana wa kufanya machaguo.

“Amerudi katika kipindi kizuri ambacho timu inamuhitaji, kila kocha anapenda kuona wachezaji wakiwa fiti maeneo yote, kwa sababu inasaidia kufanya mabadiliko mbalimbali ya kimbinu kutokana na mpinzani unayekutana naye,” amesema Katwila.

CHIR 01

Kocha huyo amesema mechi ijayo ya ligi dhidi ya Dodoma Jiji itakayopigwa keshokutwa huenda mshambuliaji huyo akacheza kutegemeana na hali itakavyokuwa siku husika.

Chirwa ni mfungaji bora wa Championship 2025-2026 akiwa na mabao 18 alipokuwa Kagera Sugar idadi sawa na Maulid Shaban aliyekuwa anaichezea Geita Gold ambapo wote kwa sasa wako timu moja.

Mshambuliaji huyo amekuwa na mwenendo mzuri na kikosi cha Geita Gold, kwani hadi sasa ameshakifungia mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara.