Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold yarudi kazini

GEITA Pict

Muktasari:

  • Geita Gold imeanza msimu wa 2026-2027 ikiwa na matokeo mchanganyiko, ambapo baada ya kucheza mechi sita imekusanya pointi saba kupitia ushindi mara mbili, sare moja na vipigo vitatu. Imefunga mabao tisa na kuruhusu manane, ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo.

GEITA Gold imeingia kwenye mapumziko ya Ligi Kuu Bara ikiwa na kazi ya kujipanga upya, huku Kocha Mkuu, Zuber Katwila akiwasha moto wa maandalizi kwa kuandaa mechi nne za kirafiki, lengo likiwa ni kupima ubora wa kikosi chake kabla ya ligi kuendelea.

Geita Gold imeanza msimu wa 2026-2027 ikiwa na matokeo mchanganyiko, ambapo baada ya kucheza mechi sita imekusanya pointi saba kupitia ushindi mara mbili, sare moja na vipigo vitatu. Imefunga mabao tisa na kuruhusu manane, ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo.

Ilianza msimu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, kabla ya kupoteza 1-0 kwa Namungo. Kisha ikafanya mambo makubwa kwa kuichapa Kagera Sugar mabao 6-2, ikafuatia sare ya 2-2 na Azam, ndipo ikapoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Simba (2-0) na Yanga (1-0).

GEIT 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Katwila amesema kikosi kimerudi mazoezini na moja ya kazi kubwa ni kuwapa wachezaji nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia mechi za kirafiki walizopanga.

“Tumerejea mazoezini na tunataka kutumia kipindi hiki kupima ubora wa wachezaji wetu. Tumepanga kucheza mechi nne za kirafiki ambazo zitatusaidia kujua kiwango cha kikosi na maeneo ambayo tunahitaji kuongeza nguvu,” amesema Katwila.

Kocha huyo amesema lengo lingine ni kuhakikisha mapumziko hayapunguzi kasi ambayo timu ilikuwa nayo katika mashindano, akisisitiza umuhimu wa kuwa tayari kabla ya ratiba ya ligi kuanza tena.

GEIT 02

“Tunataka kuwa sawa kabla ya ligi kuanza, hatutaki kupoteza kasi yetu. Hizi mechi za kirafiki zitatusaidia kuendelea kuwa kwenye ushindani na pia kuwapa nafasi wachezaji ambao wanahitaji muda zaidi wa kucheza,” amesema Katwila.

Geita Gold kwa sasa pia imepata habari njema baada ya sehemu kubwa ya wachezaji waliokuwa nje wakisumbuliwa na majeraha kurejea mazoezini. Katwila amesema hali hiyo inampa nafasi pana zaidi ya kuwapanga na kuwafanyia tathmini kabla ya ligi kurejea.

GEIT 03

“Wachezaji wetu wengi waliokuwa majeruhi wamerudi na wameanza mazoezi. Chirwa (Obrey) na wengine wapo kwenye mazoezi, isipokuwa Jackson Suluja ambaye bado anaendelea na matibabu baada ya kuumia wakati wa maandalizi ya msimu,” amesema.

Katwila aliwahi kuifundisha Mtibwa Sugar na Ihefu, anaionoa Geita Gold ambayo aliipandisha kutoka Ligi ya Championship.

Oktoba 8, 2026 ambapo Ligi Kuu Bara itakaporejea, kikosi hicho kitakuwa ugenini kucheza dhidi ya Pamba Jiji, mechi itakayopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, saa 10:15 jioni.