CAF yatoa mkeka kwa Yanga, Simba
Muktasari:
- Katika mashindano hayo Tanzania itawakilishwa na Yanga na Simba katika Ligi ya Mabingwa huku Azam na Singida Black Stars zitawakilisha katika Kombe la Shirikisho.
CAIRO, MISRI: SHIRIKISHO la Soka Afrika(CAF) imetangaza rasmi kalenda ya mechi za msimu wa 2026/27 wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika mashindano hayo Tanzania itawakilishwa na Yanga na Simba katika Ligi ya Mabingwa huku Azam na Singida Black Stars zitawakilisha katika Kombe la Shirikisho.
Msimu uliopita klabu za Tanzania ziliweka rekodi kwa zote kuvuka kucheza hatua ya makundi ya mashindano hayo, lakini zilishindwa kufuzu kwa hatua robo fainali.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, msimu wa 2026/27 utaanza kwa hatua ya kwanza ya mchujo, ambapo mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya 4-6 Septemba 2026, huku marudiano yakifanyika 11-13 Septemba 2026.
Hatua ya pili ya mchujo itaanza kwa mechi za mkondo wa kwanza kati ya 16-18 Oktoba 2026, kabla ya marudiano kuchezwa 23-25 Oktoba 2026.
Baada ya hatua za mchujo kukamilika, hatua ya makundi ya mashindano yote mawili itaanza mwishoni mwa mwezi Novemba 2026.
Ratiba ya hatua za mchujo
Hatua ya kwanza (Mkondo wa kwanza): 4–6 Septemba 2026
Hatua ya kwanza (Marudiano): 11–13 Septemba 2026
Hatua ya pili (Mkondo wa kwanza): 16–18 Oktoba 2026
Hatua ya pili (Marudiano): 23–25 Oktoba 2026
Ratiba ya hatua ya makundi
Mzunguko wa 1: 27–29 Novemba 2026
Mzunguko wa 2: 4–6 Desemba 2026
Mzunguko wa 3: 18–20 Desemba 2026
Mzunguko wa 4: 8–10 Januari 2027
Mzunguko wa 5: 15–17 Januari 2027
Mzunguko wa 6: 22–24 Januari 2027
Ratiba ya hatua za mtoano
Robo fainali (Mkondo wa kwanza): 26–28 Februari 2027
Robo fainali (Marudiano): 5–7 Machi 2027
Nusu fainali (Mkondo wa kwanza): 9–11 Aprili 2027
Nusu fainali (Marudiano): 16–18 Aprili 2027
Fainali: Itachezwa kati ya 9 Mei na 31 Mei 2027, kulingana na ratiba itakayothibitishwa na CAF baadaye.