Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yaridhishwa na maandalizi ya MOI kuelekea AFCON 2027

Muktasari:

  • AFCON 2027 itaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeeleza kuridhishwa na maandalizi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) katika kutoa huduma za tiba za michezo kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

AFCON 2027 itaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

Kauli hiyo imetolewa baada ya ujumbe wa CAF kutembelea MOI kwa ajili ya kutathmini uwezo wa taasisi hiyo katika kutoa huduma za afya, hususan zinazohusisha mifupa, mishipa ya fahamu na majeraha yanayotokana na michezo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa Huduma za Afya wa CAF, Boubakary Sidiki, amesema wamefurahishwa na maandalizi yanayofanywa na MOI.

“Huduma bora za afya ni sehemu muhimu ya kuhakikisha usalama na ustawi wa wanamichezo wakati wa mashindano makubwa kama AFCON,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa MOI, Dk Asha Abdullah, amesema taasisi hiyo iko tayari kutumia utaalamu na uwezo wake kushirikiana na CAF pamoja na wadau wengine wa michezo katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa tiba za michezoni.

“MOI iko tayari kushirikiana na CAF na wadau wote kuelekea AFCON 2027. Tunaamini maandalizi haya ni fursa ya kuimarisha huduma za tiba za michezoni na kuhakikisha wanamichezo wanapata huduma bora, salama na kwa wakati,” amesema.