Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco ndio basi tena Simba

SAFARI ya misimu saba ndani ya Simba kwa mshambuliaji John Bocco inakaribia ukingoni baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtoa kwenye mipango yao ya msimu ujao.

Simba sasa inajiandaa kuachana na wachezaji wake wasiopungua watano kwenye dirisha dogo hili la usajili huku wengine wakisubiriwa mwisho wa msimu ufike wamalize mikataba yao na kuondoka huru.

Mwanaspoti limethibitisha, uongozi wa Simba tayari umemalizana na Bocco kwa kumpa uhuru wa kuchagua kuondoka Msimbazi kwenye dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kama ikishindikana basi atasubiri hadi mwisho wa msimu mkataba wake umalizike aondoke.

Tayari staa huyo aliyeingia Msimbazi mwaka 2017 akitokea Azam, ametolewa kwenye mipango ya kocha mpya Abdelhak Benchikha na sio sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Morocco kwaajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wydad AC itakayopigwa Jumamosi wiki hii.

Akiwa Simba, Bocco alitwaa mataji manne ya ligi mfululizo kuanzia msimu wake wa kwanza unyamani 2017/2018 hadi 2021/2022 pia kwa nyakati tofauti amekuwa mshambuliaji kinara akiibuka mfungaji bora wa ligi msimu wa 2020/2021 (mabao 16).