BlackSailors yatambia usajili
Muktasari:
- Klabu hiyo yenye historia katika soka la Zanzibar imekuwa ikijenga kikosi chenye mchanganyiko wa vijana wenye vipaji na wachezaji wenye uzoefu. Timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu imeendelea kujiweka sawa kwa kuo ngeza wache zaji wapya kwenye kikosi hicho.
TIMU ya ya BlackSailors imeanza hatua mpya ya maandalizi kwa kuwatambulisha wachezaji wake watakaokuwa sehemu ya kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Klabu hiyo yenye historia katika soka la Zanzibar imekuwa ikijenga kikosi chenye mchanganyiko wa vijana wenye vipaji na wachezaji wenye uzoefu. Timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu imeendelea kujiweka sawa kwa kuo ngeza wache zaji wapya kwenye kikosi hicho.
Wachezaji ambao wametambulishwa na timu hiyo ni pamoja na Moh’d Said ‘Wakufosi’, Ismail Haji Mwinyi ‘Isma’, Yassir Said Malik ‘Thiago’, Said Omar ‘Natepe’ na Baaraka Saidi.
Akizungumza baada ya kujiunga na timu hiyo, Baraka amesema anafuraha kujiunga kwenye timu hiyo na ataitumikia kwa nguvu zake zote. Amesema, ataipambania timu hiyo kwa umoja wao kwa kushiriakiana na wachezaji wenzake na hatokwenda kinyume cha makubaliano yao.
“Karibuni kwenye familia ya mabaharia weusi, huku kwetu ni furaha na waambieni kuwa watatubu msimu huu,” ilisema taarifa ya kuwakaribisha wachezaji wao.
Pia, taarifa hiyo ilisema kuwa timu hiyo imeshatoa fedha zake benki kutafuta wachezaji wenye viwango na watakaoitumikia timu hiyo kwa kila hatua.
Black Sailors, ambayo imewahi kushiriki Ligi Kuu Zanzibar, sasa inalenga kujenga msingi imara wa ushindani na kurejea kwenye nafasi ya juu ya soka