Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Black Sailors kazi imeanza

BLACK Pict

Muktasari:

  • Benchi la ufundi linaamini kuwa kupitia maandalizi haya, ushirikiano wa wachezaji na nidhamu ya mazoezini, timu hiyo itakuwa tayari kutoa ushindani mkubwa pindi msimu mpya utakapoanza Agosti 29, 2026.

KLABU ya Black Sailors imeendelea na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Zanzibar kwa kasi huku benchi la ufundi likieleza kuridhishwa na mwitikio wa wachezaji mazoezini.

Hata hivyo, licha ya kikosi hicho kuanza mazoezi, bado hakijakamilika kutokana na baadhi ya wachezaji waliotoka Tanzania Bara kutokuwasili Zanzibar.

Kocha wa timu hiyo, Mohammed Ali Hilal ‘Tedy’ amesema hali ya kikosi inaendelea kuimarika na wachezaji wanaonesha nidhamu, ari ya kujifunza na utekelezaji mzuri wa maelekezo yanayotolewa na benchi la ufundi.

Amesema, jambo linalompa matumaini makubwa ni namna wachezaji wapya pamoja na waliokuwepo msimu uliopita wanavyoshirikiana, hali inayorahisisha kujenga kikosi chenye ushindani na kuelewana mapema kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

“Tunafanya mazoezi katika mazingira mazuri na wachezaji wanapokea vizuri maelekezo tunayowapa, hilo linatupa imani kwamba tutafikia kiwango tunachokihitaji kabla ya ligi kuanza,” amesema Tedy.

Amesema, matarajio ya benchi la ufundi ni kwamba kuanzia Jumatatu ijayo wachezaji wote waliokuwa wakisubiriwa watakuwa wamewasili, jambo litakalowezesha kuendelea na programu ya maandalizi ikiwa na kikosi kamili pamoja na kuongeza kiwango cha ushindani ndani ya timu.

Benchi la ufundi linaamini kuwa kupitia maandalizi haya, ushirikiano wa wachezaji na nidhamu ya mazoezini, timu hiyo itakuwa tayari kutoa ushindani mkubwa pindi msimu mpya utakapoanza Agosti 29, 2026.