Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bihimba Cup 2021 mapema tu Julai

Dar es Salaam. Vijana wametakiwa kujiingiza katika michezo ikiwemo mpira wa miguu ili kuepukana vitendo vya kiharifu ikiwemo uvutaji wa dawa za kulevya na wizi

Akizungumza hayo leo Juni 8, 2021 mwandaaji, Bihimba Mpaya wakati akiitambilisha ligi ya mpira wa miguu 'Bihimba Cup 2021' inayotarajiwa kuanza Julai mwaka huu katika viwanja vya shule ya Msingi Kivule ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa

Mpaya alisema ligi hilo linawakutanisha vijana wa Kata ya Kivule wa mtaa Kivule, Bombambili, Kerenzange na Magole A kwa lengo vijana hao waonyeshe vipaji vyao na kuachana na vitendo vya uhalifu.

Alisema vijana hao wataonyesha vipaji vyao ambavyo vitaonekana na kusajiliwa katika timu kubwa za hapa nchini na nje ya nchi.
Bihimba alitolea mfano wa Bwana Samata ambaye kwa sasa anachezea timu Fenerbahce nchini Uturuki alianzia timu ya Mbagala Marketing baadaye alisajiliwa Simba Sport Club na TP Mazembe ya nchini Congo.

"Mwaka 2017 nilishawahi kuanzisha ligi la Ng'ombe Cup na lilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi ya Kivule na mwaka huu mchezo wa mpira wa miguu utafanyika katika viwanja hivyo vya shule ndani ya mwezi mmoja tutaanza na mzunguuko, halafu robo fainali, nusu fainali na fainali," alisema Bihimba

Bihimba alisema mshindi wa kwanza atasepa na ng'ombe mzima na wa pili atapata jezi seti mbili na mshindi wa tatu atapata mipira miwili huku mfungaji bora akijinyakulia sh 100,000.