Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Betika yahamasisha utunzaji mazingira kupitia Ligi ya Sodo

Timu nane zinachuana kusaka bingwa wa mashindano maalumu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira yaliyoandaliwa na Kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania ya Betika.

Ligi hiyo iliyopewa jina la Betika Sodo 4 Climate, mbali na uwanjani, pia inawahamasisha  washiriki na jamii utunzaji wa mazingira  kupitia mchezo wa sodo.

Meneja mkuu wa Betika Tanzania, Tumaini Maligana
Ligi hiyo ina kauli mbiu ya Shabikia soka sio  uharibifu wa mazingira.

"Lengo ni kushiriki katika kutokomeza uharibifu wa mazingira unaosababisha pia athari za mabadiliko ya tabia za nchi.

"Tunapotunza mazingira  tunakuwa na hali ya hewa nzuri, afya bora na pia maendeleo katika jamii yetu," amesema.

Kuhusu Betika Sodo 4 Climate, Maligana amesema Ligi hiyo inafachezwa kwenye fukwe za Coco ikishirikisha timu nane ambazo zitachuana kwa wiki saba.

Timu hizo ni Betika staff,  Coco beach,  RC FC , Tulia Trust Foundation. Espanyol,  Bodaboda Msasani na IPP Media.

"Timu hizo pia zitakuwa na timu za wanawake, kila jumamosi kutakua na mechi moja ya wanawake na mechi moja kwa wanaume," amesema.

Ufunguzi wa Ligi hiyo jana ulitanguliwa na usafishaji wa mazingira na kutoa elimu kuhusiana na swala zima la kuhifadhi taka katika maeneo husika.

Mechi ya ufunguzi  Betika staff  ilichapwa mabao 3-1 na  Coco Beach FC.

Mbali na mechi, katika kipindi cha wiki zote saba za ligi hii kutakua na matukio mbali mbali, huku mabingwa wakitarajiwa kuondoka na zawadi mbalimbali kutoka Betika.