Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benchi jipya Yanga moto

MASHABIKI wa soka wa Yanga kwa sasa hawana wanachotaka kusikia zaidi ya kulijua jina la kocha mkuu mpya wa kuchukua nafasi ya Cedric Kaze aliyesitishiwa mkataba wake wiki iliyopita, lakini kazi ya kulipata jina moja la fundi huyo wa kuibeba timu hiyo imewatoa jasho mabosi wao.

Mara baada ya Kaze kutangazwa kutemwa saa chache tangu Yanga ilipolazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Jumapili iliyopita, fasta makocha wa nchi mbalimbali wakiwamo Watanzania walichuana kutuma maombi na cv zao ili kuomba kazi.

Hata hivyo mpaka kufikia Ijumaa kulikuwa na jumla ya makocha 75 walioomba kazi Jangwani na mabosi wa klabu hiyo wakaitana ili kupitia majina yao kwa lengo la kumpa mmoja wa kuwafaa na hadi jana tayari walikuwa wamekabisha majina matano.

Mabosi hao wakatamka kwamba hawatamaliza wiki ijayo watakuwa wameshapata bosi mpya mkuu wa ufundi katika kikosi chao kinachoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 23 na kukusanya alama 50, nne zaidi na walizonazo watani wao, Simba wanawafuata nyuma yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa Yanga, Dominic Albinius ‘Baba Paroko’ amelithibitishia Mwanaspoti kwamba wako makini katika mchakato wa kumsaka mrithi wa Kaze na kwamba kwa sasa wamesaliwa na majina matano ambayo wanaendelea kuyachekesha kupata moja wanalohitaji.

“Tupo makini sana na tunahitaji utulivu sana katika maamuzi ya muda huu tunataka kupata kocha sahihi na muafaka kwa klabu yetu kulingana na malengo yetu ya msimu huu na ikiwezekana huko mbele,” alisema Albinius.

Albinius alisema wamebakiza makocha watano ambao sasa wanaingia katika mchujo mwingine ambao ulitarajiwa kufanyika jana jioni ili kupata wawili au watatu wa mwisho.

“Tumeshatoka huko kwenye makocha zaidi ya 70 na sasa tumebakiza watano na mchakato bado unaendelea tunalazimika kumaliza vikao muda mbaya sana ili tu tuweze kupata mtu mmoja ambaye atakuwa sahihi,” alisema Albinius na kuongeza;

“Kati ya hawa watano tunataka kubaki na makocha watatu au ikiwezekana wawili ambao tutakwenda nao katika uamuzi wa mwisho. Tunapambana kuhakikisha kabla ya wiki ijayo haijamalizika kocha awe kambini na wachezaji wake tayari kwa kazi,tupeni muda tufanye kazi ya wananchi.”

Wakati Albinius akiyasema hayo Mwanaspoti linafahamu kwamba mabosi wa Kamati ya Utendaji jana walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu wapitishe uamuzi wa kuwafuta kazi makocha wao Cedric Kaze na wasaidizi wake Nizar Khalfan na Vladimir Niyonkuru.

Inaelezwa kwamba Albinius ndiye ambaye angeweza kutoa mwanga wa kamati yake katika mchakato wa warithi wa makocha hao kwa kamati hiyo kabla ya uamuzi wa mwisho, huku majina ya makocha wenye rekodi zao Ulaya na Afrika yakitajwa akiwamo Kocha wa zamani wa TP Mazembe, Mfaransa Hubert Velud na Patrick Aussems wa AFC Leopards.

Hakuna kiongozi yeyote wa Yanga akiwamo Albinius aliyekuwa tayari kuaminika majina hayo matano ya mwisho ambayo ndimo litakalotoka moja la kuja kuchukua nafasi ya Kaze aliyedumu Jangwani kwa siku 142 tangu aliposaini mkataba Oktoba 16 mwaka jana.