Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki wa Simba mdogo mdogo

BEKI wa kati wa Simba anayecheza kwa mkopo ndani ya Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame aliyekuwa nje ya uwanja tangu alipoumia kwenye pambano la Ligi Kuu dhidi ya Yanga lililopigwa Februari 23 ameanza kurejea kwa kufanya mazoezi mepesi.

Ame alishindwa kupata nafasi ndani ya Simba na kutolewa kwa mkopo katika dirisha dogo, amesema maumivu ya goti yalimnyima raha tangu alipoumia katika mchezo huo wa Yanga uliopigwa Uwanja wa Manungu na Mtibwa kulala mabao 2-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ame alisema baada ya kurudi kambini na kutulia aliona goti lake limevimba na kusikia maumivu makali hata kushindwa kutembea sawa sawa kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kuumia.

“Nilipewa mapumziko na timu kwa ajili ya kupata muda wa kuendelea na matibabu ilinibidi nirudi nyumbani Zanzibar tangu wakati huu hadi sasa nipo huku nikiendelea kujiuguza,” alisema Ame na kuongeza;

“Baada ya kufika hapa nyumbani na kufanya vipimo hospitali niligundulika ligamenti ndogo imekatika na nikapewa matibabu ya kufanya na nashukuru wakati huu maendeleo yangu ni mazuri.

“Rasmi nimeanza mazoezi binafsi gym baada ya hapo nitarudi tena hospitali nitapangiwa ratiba nyingine ya kwenda kukimbia bechi kwenye mchanga mwingi nikiwa bila ya viatu.”

Aliongeza kwa kusema; “Nikimaliza hiyo programu ya bechi nitarudi hospitali kwa uangalizi wa mwisho kisha nitapewa ruhusa ya kujiunga na timu kuendelea na ratiba zao na mabo yote haya ili kuwa sawa nadhani ni ndani ya mwezi mmoja tu.”