Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beach Volleyball kuibua vipaji Zanzibar

KATIBU Msaidizi wa mchezo wa Beach Volleyball, Eustice Mwakanjuki, amewataka wanamichezo kutumia fursa ya kuwavutia vijana ili kuwaepusha na makundi yasiyofaa katika jamii.

Amesema, michezo ina nafasi kubwa katika kuwaweka vijana mbali na makundi yasiyofaa, hivyo wanamichezo wanapaswa kuwa mabalozi wazuri kwa vijana wengine kushiriki michezo.

“Beach volleyball ni miongoni mwa michezo inayoweza kuwa na mchango kuwahamasisha vijana, kutokana na mazingira yake na namna inavyowapa washiriki fursa ya kufanya mazoezi huku wakijenga afya na uhusiano mwema,” amesema.

Pia, aliwataka wachezaji kutumia nafasi hiyo kuutangaza mchezo huo kwa vijana wengine ili kuondoa dhana potofu kwamba ni mchezo usio na umuhimu.

Amesema, licha ya Beach Volleyball kuchezwa na wachezaji wawili kwa kila upande, mchezo huo umeonesha ushindani mkubwa na kuwavutia mashabiki wanaofutilia.

Pia, katibu huyo amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za mchezo na dhana ya mchezo wa kiungwana na kuwataka wanamichezo kuendelea kudumisha nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Alieleza kuwa, ushiriki wa wanamichezo katika matamasha unaongeza hamasa na kutoa fursa kwa wananchi na vijana.