Bashungwa aipa pole Simba, familia ya Hans Poppe
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameguswa na kifo cha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Zakaria Hans Poppe na kutoa pole kwa klabu hiyo.
Bashungwa kupitia Instagram ameandika;
"Natoa pole kwa uongozi na mashabiki wa Simba kufuatia kifo cha Zakaria Hans Poppe. Nimeipokea taarifa ya msiba huu kwa mshtuko na masikitiko kwani mchango wake katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini ni mkubwa na ulikuwa bado unahitajika katika kipindi hiki ambacho timu zinabadili mfumo kujiendesha kibiashara zaidi,"
"Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi na kuipa familia yake moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu,"