Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker azifuata dakika 90 za Yanga, Azam

BARKER Pict

Muktasari:

  • Barker mapema tu alitua Uwanja wa Amaan akiwa na wasaidizi wake hao wawili na makomandoo wawili wa Simba na walikwenda kukaa moja kwa moja kwenye majukwaa ya pembeni wakijichanganya na mashabiki.

WAKATI Yanga ikiwa uwanjani dhidi ya Azam basi jukwaani kulikuwa na makocha watatu wa Simba akiwemo bosi wao, Steve Barker na wasaidizi wake wawili wakizisoma timu hizo mbili.

Barker mapema tu alitua Uwanja wa Amaan akiwa na wasaidizi wake hao wawili na makomandoo wawili wa Simba na walikwenda kukaa moja kwa moja kwenye majukwaa ya pembeni wakijichanganya na mashabiki.

Wakati mwingi Barker akiwa jukwaani na wasaidizi wake alionekana kubadilishana mawazo na wenzake huku mwingine akinakili mazungumzo yao kwenye karatasi ndogo kwa siri.

Akiwa jukwaani hapo, Barker alikutana na wakati mgumu pale ambapo Yanga ilipata bao na mashabiki wa mabingwa hao watetezi wa kombe hilo la Muungano walimkebehi wakimwambia bado Simba.

Wakati mashabiki hao wakipeleka ujumbe huo, Barker hakuonyesha kuchukizwa na muda wote alikuwa akiwaonyesha tabasamu kisha kuwauliza walinzi wake maana ya kile ambacho walikuwa wanasema.

Azam iliporuhusu bao la pili Barker alionyesha kutabasamu pia huku akisikitika kidogo na kuendelea kutazama mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Muungano ambao Yanga ilishinda mabao 2-1.

Kocha huyo hakukaa hadi mwisho na mara baada ya Azam kupata bao dakika tano baadaye aliondoka uwanjani hapo kimyakimya huku mashabiki wa Yanga wakimshangilia.

Mashabiki hao walikuwa wakimkebehi kwa kauli mbalimbali zikiwemo 'bado Simba' lakini wengine wakimwambia Simba isikimbie ishinde wakutane kwenye fainali na wakati wote kocha huyo raia wa Afrika Kusini alikuwa akicheka.

Mara baada ya kutoka nje ya uwanja, Barker hakuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusu alichokiona kwenye mechi hiyo na aliingia kwenye gari na wasaidizi wake kisha kuondoka haraka uwanjani hapo.

Simba leo usiku itakuwa uwanjani kwa mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Mlandege ya Zanzibar, itakayoamua nani anakwenda kukutana na Yanga kwenye fainali, Aprili 29,2026.