Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraza: Simba? wepesi waje tu

ACHA waje. Ni neno la Kocha Mkuu wa Biashara United, Francis Baraza alilotamka wakati akiwaambia Simba kuwa wasitarajie mteremko kwenye mchezo wao unaopigwa Alhamisi mjini Musoma.

Biashara United imekuwa moto kwenye Ligi Kuu ikitembeza vipigo ambapo Alhamisi ya wiki hii itakuwa nyumbani kukipiga dhidi ya bingwa mtetezi Simba katika dimba la Karume mjini mjini Musoma.

Wakati timu hizo zinakutana, kila upande una kumbukumbu ya ushindi katika mchezo wake uliopita, ambapo Simba iliitandika AS Vita katika mechi ya klabu bingwa Afrika na Biashara United wakiilalua Mwadui mabao 2-1 ikiwa mjini Shinyanga.

Baraza alisema hana hofu yoyote juu ya wapinzani kwani anaamini kwa ari na uwezo wa nyota wake wataizima Simba ikiwa na kikosi chake wakiwamo nyota wake wa kimataifa.

Alisema Biashara United ni timu kama zilivyo nyingine Ligi Kuu na kwamba hata kama watahitaji kuja leo au kesho waje tu, huku akitamba kuwa msimu huu wana jambo lao.

“Waje tu hata kesho, sisi tuko tayari kimapambano kila mchezo una umuhimu sana kwetu katika kufikia malengo yetu msimu huu, hatuna hofu wala kuogopa timu yoyote” alisema Baraza.

Kocha huyo raia wa Kenya aliongeza kuwa licha ya kwamba mechi hiyo itakuwa na upinzani kutokana na ubora wa kila timu, lakini anaamini kwa kiwango walichoonesha vijana wake lazima wafanye kweli.

“Ushindi tuliopata dhidi ya Mwadui na kiwango walichoonesha nyota wangu naamini tutandeleza pale pale, kimsingi ni kuwaandaa vijana wangu kisaikolojia” alisema Kocha huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwenye ligi hiyo kwa sasa.