Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI achekelea dabi, ataja bingwa Bara

AZIZ Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita alipotupia mabao 21, ameondoka nchini akiwa na kumbukumbu nzito kwa mashabiki wa timu hiyo aliotokea kuwa kipenzi chao kutokana na namna alivyokuwa akilipigania jahazi lao.

MWAMBA wa Burkina Faso, Stephanie Aziz KI tayari ameshaanza kukipiga katika chama lake jipya la Wydad Casablanca alikotua hivi karibuni akitokea Yanga, lakini huku nyuma kaacha kumbukumbu kibao Jangwani anazotembea nazo.

Nyota huyo aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita alipotupia mabao 21, ameondoka nchini akiwa na kumbukumbu nzito kwa mashabiki wa timu hiyo aliotokea kuwa kipenzi chao kutokana na namna alivyokuwa akilipigania jahazi lao.

Akiwa nchini Marekani ambako Wydad inashiriki fainali za Kombe la Dunia la Klabu, Aziz KI amepiga stori na Mwanaspoti akichekelea suluhu iliyopatikana kwa kurejeshwa   mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliopangwa kupigwa Juni 25 kati ya timu yake ya zamani, Yanga dhidi ya Simba kisha akatabiri ubingwa.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Marekani, Aziz KI alisema hatua ya kupatikana muafaka wa mchezo huo imemfurahisha akishusha presha kwa timu yake kujiondoa kwenye uwezekano wa kupoteza ubingwa msimu huu.

Aziz KI alisema hatua ya Yanga kurudi mchezoni na mechi hiyo kupigwa Juni 25 anaamini kwamba mabingwa hao watetezi watautetea ubingwa huo.

“Nimesikia kwamba muafaka umepatikana ni habari njema. Nimefurahia hilo. Wakati naondoka kulikuwa na huo wasiwasi wa kuchezwa hiyo mechi, ilikuwa inanitisha nikiona kama mchezo hautapigwa Yanga ingeweza kupoteza ubingwa,” alisema Aziz KI.

“Ubingwa ungeweza kwenda Simba hii isingekuwa nzuri kwangu. Uliona namna msimu huu ulivyokuwa na mambo mengi, tulikuwa na kuanguka na kuinuka na tulijituma kurudi mchezoni.

“Kuna wakati niliwaambia wachezaji wenzangu kwamba licha ya mechi ambazo tulipoteza msimu huu na kutupunguza kasi, lakini mwisho tulitakiwa kuupigania ubingwa hilo  ndio muhimu na sasa naona matumaini.

“Kama Yanga ikicheza hiyo mechi nina uhakika watashinda na itakuwa bingwa, sina wasiwasi na ubora wa wachezaji wenzangu wala makocha niliowaacha.”

Nyota huyo aliwataka wachezaji wenzake kupambana kwani mechi mbili zilizosalia hazitakuwa rahisi kwa kuwa wanacheza na timu zinazotaka pia ushindi ili zijiweke vizuri kwenye msimamo wa ligi.

Mchezaji huyo alisema mchezo dhidi ya Simba ambao utakuwa wa mwisho kwenye ligi utakuwa sawa na fainali nyingine kabla ya kucheza ile ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars mechi itakayopigwa Juni 28 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, Zanzibar.

“Mchezo dhidi ya Simba hautakuwa rahisi, utakuwa mgumu na umeona imekuwa mechi ya mwisho. Kwa hiyo inahitajika kucheza mechi hizi tatu kwa hesabu kubwa,” alisema Aziz KI kabla ya mechi ya jana.

Jana usiku mchezaji huyo alitarajiwa kuwepo uwanjani wakati Wydad ilipokuwa ikivaana na Manchester City ya England katika mechi ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu zinazoendelea nchini Marekani.