Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arthur Melo: Fundi mpya Barcelona aliyezima Real Madrid

Muktasari:

  • Maskauti wa Klabu ya Gremio inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil mwaka 2010, walimuona mmoja kati ya mastaa wa Barcelona walioimaliza kabisa Real Madrid katika pambano la wikiendi iliyopita, Arthur Melo ambaye jina lake linazidi kuvuma kwa kasi Nou Camp tangu atue. Maskauti hao walimwona Melo  katika michuano ya vijana na kufanikiwa kumnasa.

BARCELONA, HISPANIA .MMOJA kati ya mastaa wa Barcelona walioimaliza kabisa Real Madrid katika pambano la wikiendi iliyopita ni staa mpya wa Barcelona, Arthur Melo ambaye jina lake linazidi kuvuma kwa kasi Nou Camp tangu atue klabuni hapo katika dirisha kubwa la majira ya joto akitokea Gremio. Ni nani huyu Arthur?

Aibuliwa na Luiz Felipe Scolari.

Jina lake halisi ni Arthur Henrique Ramos de Oliveira Melo na alizaliwa Agosti 12, 1996 katika eneo la Goiania nchini kwao Brazil. Arthur alianza kucheza soka katika klabu ya mtaani kwao ya Goias akiwa na umri wa miaka 12.

Hata hivyo, mwaka 2010 maskauti wa klabu ya Gremio inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil walimuona katika michuano ya vijana na kufanikiwa kumnasa. Januari 2015 baada ya kutesa katika michuano ya vijana ya jimbo la Sao Paulo, Arthur alipelekwa katika kikosi cha kwanza na kocha wa Gremio, Luiz Felipe Scolari.

Bila ya kutazamia alicheza mechi yake ya kwanza katika michuano ya Jimbo dhidi ya Aimoré. Hata hivyo alitolewa wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na mlinzi wa Argentina, Matias Rodriguez. Hakucheza tena mechi za wakubwa msimu huo.

Mwaka 2016, Arthur alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi katika pambano Botafogo walilochapwa 1-0 akiingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kaio katika kipindi cha pili. Mwaka 2017 alikuwa mchezaji wa kudumu katika kikosi cha kwanza.

Katika pambano lake la kwanza la klabu bingwa Amerika Kusini maarufu kama Copa Libertadores lililoisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Guarani, Arthur alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya kufikisha pasi zote 40 alizopiga.

Alifunga bao lake la kwanza katika soka la kulipwa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fluminense kombe la Brazil. Julai alifunga bao lake la kwanza la Ligi katika ushindi wa mabao 3-1 wa Gremio ugenini dhidi ya Vitoria.

Afananishwa na Iniesta, Barca yamnasa

Aina yake ya soka imekuwa ikilinganishwa zaidi na viungo mahiri wawili wa Hispania, Andrés Iniesta na Thiago Alcântara. Arthur ana kipaji kikubwa katika umiliki wa mpira pamoja na kupiga pasi fupi na ndefu ambazo zimempatia umaarufu mkubwa.

Klabu kubwa za Ulaya, Chelsea, Manchester United na Barcelona zote zilikuwa zinamfukuzia kwa karibu Arthur lakini ni Barcelona ndio ambao walifanikiwa kuinasa saini yake kwa dau la Euro 40 milioni.

Kabla ya hapo Kocha wa United, Jose Mourinho aliwatuma maskauti wake kwenda kutazama kipaji cha Arthur huku Chelsea nayo ikimtazama kwa karibu lakini kwa mujibu wa Mwandishi nguli wa soka la Hispania, Guillem Balague atoa siri kwamba Barcelona wamefikia makubaliano ya kumnasa kinda huyo.

“Arthur ana makubaliano na Barcelona, lakini inahitaji kuthibitishwa na Gremio ambayo inataka ilipwe kiasi cha Pauni 44 milioni kwa ajili ya kumruhusu aondoke. Kiasi hicho kipo katika kipengele cha mkataba wake.” alisema Balague.

Taarifa nyingine zilidai kwamba siku mbili baada ya kuisaidia Gremio kutwaa taji lake la tatu la Copa Libertadores, Arthur pamoja na wakala wake, Andre Curry walikutana na Maofisa wa Barceona katika mji wa Porto Alegre kujadili zaidi uhamisho wa staa huyo.

Hata hivyo utata ulizuka baada ya picha kuibuka zikimuonyesha Arthur akiwa na jezi ya Barcelona kando ya Baba yake, wakala wake na mfanyakazi mmoja wa wakala wake. kitu hicho kiliichukiza Gremio ambayo ilisisitiza kwamba staa huyo angeondoka kwa dau lililopo katika mkataba wake tu ingawa Barcelona walitaka kulipa dau la chini.

baadaye Gremio ilisisitiza kwamba isingemruhsu nyota huyo kuondoka Brazil kabla ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Russia mapema mwaka huu

Machi 11, 2018, Barcelona ilifikia makubaliano na Gremio kuhusu uhamisho wake kwenda Nou Camp na alisaini mkataba wa miaka sita huku akilazimika kusubiri mpaka Julai 9, 2018 kuwa mchezaji rasmi wa Barca. Alicheza mechi yake ya kwanza kwa Barca katika pambano la maandalizi ya msimu dhidi ya Tottenham mnamo Julai 28 na kufunga bao lake la kwanza katika pambano hilo.

Yumo kikosi cha Brazil

Arthur ameichezea Brazil katika ngazi zote. Ameichezea katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17 na kile cha chini ya umri wa miaka 20. Alikuwa seheu ya kikosi cha Brazil chini ya umri wa miaka 17 kilichoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Amerika Kusini chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2013.

Septemba 15 mwaka huu, Arthur baada ya kung’ara zaidi na kikosi cha Gremio aliitwa katika kikosi cha wakubwa cha Brazil ambacho kilitarajiwa kucheza mechi mbili za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Bolivia na Chile.

Arthur alikuwepo katika kundi la wachezaji wa akiba kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia nchini Russia mapema mwaka huu. hakuweza kwenda Russia kutokana na timu hiyo kupata majeruhi katika eneo la kiungo.