Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aman Josiah aona kitu Mashujaa

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Josiah ambaye amejiunga na Mashujaa msimu huu akitokea Dodoma Jiji aliyoisaidia kumaliza nafasi ya tisa katika Ligi Kuu Bara 2025-2026, amesema timu hiyo imecheza mechi saba za kirafiki zilizomsaidia kuwajenga wachezaji kimbinu huku wapya wakielewana na wenzao.

WAKATI Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026-2027 ikitarajia kuanza leo, Ijumaa Agosti 14, 2026, Kocha wa Mashujaa FC, Aman Josiah amezungumzia maandalizi ya kikosi chake huku akibainisha tayari anaona mastaa wake wameanza kuingia katika mfumo wa mbinu zake.

Josiah ambaye amejiunga na Mashujaa msimu huu akitokea Dodoma Jiji aliyoisaidia kumaliza nafasi ya tisa katika Ligi Kuu Bara 2025-2026, amesema timu hiyo imecheza mechi saba za kirafiki zilizomsaidia kuwajenga wachezaji kimbinu huku wapya wakielewana na wenzao.

“Kwa haya maandalizi nadhani mechi tulizocheza morali ipo vizuri kwa wachezaji pia maelekezo yangu wanayafuata, hivyo nina imani nao tutafanya vizuri,” amesema kocha huyo.

MASHU 01

Pia kocha aligusia juu ya uwepo wa majeruhi katika kikosi chake ambapo hata hivyo amesema haitaathiri kitu kulingana na kikosi chake kuwa kipana, huku akimtaja Mundhir Vuai kuanza kurejea mazoezini kutoka katika majeraha.

MASHU 02

“Majeruhi wapo nafikiri wanarejea kama wakina Mundhir Vuai nipo nae mazoezini lakini nafikiri waliokuwepo wana utayari, wapo kwenye afya njema,” amesema.

Mashujaa FC itaanza msimu wa 2026-2027 kwa kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union, Jumamosi Agosti 15,2026, itakayochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.