Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyepigwa ngumi na Neymar Jr afunguka

Muktasari:

  • Nelson amezungumza na Gazeti la L’Equipe kuhusu yanayomtokea tangu wakati huo.

PARIS,UFARANSA.NELSON, jamaa ambaye alipigwa ngumi na Neymar baada ya fainali ya Coupe de France, amevunja ukimya na kuelezea tukio hilo, ikiwamo yanayomkabili tangu hapo.

Shabiki huyo alikuwa akiwaporomoshea maneno machafu wachezaji wa PSG wakati wakipokea medali zao za ushindi wa pili, lakini Neymar alishindwa kuvumilia, akamchapa konde.

Nelson amezungumza na Gazeti la L’Equipe kuhusu yanayomtokea tangu wakati huo.

GAZETI: Kwanini umeamua kufunguka?

NELSON: Kuwajibu wote walionituhumu kuwa nataka pesa kutokana na tukio hili. Sijaomba hata senti. Kama ningetaka kweli ninanufaika kupitia tukio hili, ningefungua kesi, lakini sijafanya hivyo. Mtu pekee niliyeamua kumshitaki ni mwandishi wa ‘kolamu’ gazetini, Pierre Menes, kwa maoni aliyotoa kuhusu mimi. Pesa haziwezi kunipa furaha. Zitanisaidiaje kama nitapoteza heshima yangu? Kumekuwapo na matukio ya watu kunishambulia nyumbani kwangu.

GAZETI: Kuna matukio yoyote yaliyokuandama...baada ya maneno ya Mwandishi Pierre Menes?

NELSON: Napaswa kuuawa mbele ya nyumba yangu ili atambue ‘usiriaz’ wa kile alichosema? Vyombo vya habari vimekemea kitendo cha Neymar, siyo kauli zangu, lakini leo naishi kwa kughasiwa na baadhi wanafikia kuzusha nilimtolea maneno ya kibaguzi.

GAZETI: Kuna vitisho vyovyote ulivyopata nyumbani kwako?

NELSON: Watu wamesambaza anuani ya mahali ninapoishi katika mitandao ya kijamii, jambo ambalo limevuka mipaka. Mimi ni mtu ninayependa maisha na kufanya mitoko, lakini sijatoka nyumbani kwa wiki nzima. Huwa natoka, lakini si peke yangu. Alhamisi, watu wanne walinifuata na kusema, “utatukoma.”

GAZETI: Unajutia?

NELSON: Hakika najutia kwa nilichokisema, lakini hayakuwa maneno ya kuamsha hasira. Mashabiki hucheka, tunatania, tunafurahia; ndivyo mambo huwa. Najutia maneno yangu niliyoyatoa kwa (Marco) Verratti na (Gianluigi) Buffon, lakini Neymar hakupaswa kunipiga. Yeye ni mweledi na ni kawaida wao kukutana na maneno ya vile.

GAZETI: Una ujumbe gani kwake?

NELSON: Ninachotaka tukutane ili tuweke mambo sawa, nimuombe radhi na tupeane mikono. Unapata picha hivi ingekuwaje kama ni mimi ndiye ambaye ningekuwa nimempiga ngumi? Kingenitokea nini? Nataka kutembea mitaani bila ya mashabiki damu wa PSG kunivamia, au niwapeleke wazazi wangu kuutembelea Mnara wa Eiffel Tower bila ya kushambuliwa.

ALVES AMCHANA NEYMAR

Mchezaji mwenzake Neymar klabuni PSG, ambaye pia ni Mbrazili mwenzake, Dani Alves, amekosoa tukio la straika huyo baada ya timu hiyo kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Rennes.

“Kilikuwa ni kipindi kigumu kwa sababu ya kile tulichokipata,” Dani Alves aliliambia Gazeti la L’Equipe.”Kulikuwa na mzozo mkali, lakini haikupaswa kuwa vile na hakupaswa kumpiga shabiki yule. Tutalitumia tukio lile kama somo. Licha ya urafiki wetu, sisapoti alichokifanya na hatafanya tena.

“Kipigo kilituvuruga sana PSG, ambao hatujazoea kukosa mataji ya ndani. Ila tunapocheza mechi nyingi na michuano mingi sana, inakuwa ngumu kutimiza malengo.

Neymar, tangu amejiunga na PSG kwa ada ya uhamisho ya Euro 222 milioni, amefunga magoli 50 katika 57 alizocheza ndani ya misimu miwili.