Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Ahly, Esperance ni mechi ya kisasi

MABINGWA watetezi wa Klabu bingwa Afrika Al Ahly wanashuka dimbani kesho Juni 26 dhidi ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa pili wa marejeo kwenye uwanja wa Al Salam, mjini Cairo baada ya mchezo wa kwanza Al Ahly kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa nchini Tunisia.

Mchezo huo unawahitaji Al Ahly kupata ushindi au  sare ya aina yoyote ili kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwanaspoti inakuletea makala muhimu kuhusiana na timu hizi mbili.

TAKWIMU

Esperance; imecheza mechi 10  (ushindi mechi tano, sare tatu , kupoteza michezo miwili , magoli ya kufunga 14 , magoli ya kufungwa 10)

Kwenye hatua ya awali Esperance iliifunga timu ya Ahly Benghazi ya Libya mabao 3-2 kwa ujumla.

Esperance ilikuwa kwenye kundi D pamoja na  Zamalek (Misri), MC Alger (Algeria) na Teungueth (Senegal) na Esperance walimaliza kundi lao wakiwa vinara wakiwa na pointi 11, baada ya kushinda michezo mitatu, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Kwenye hatua ya robo fainali Esperance waliifunga  CR Belouizdad ya Algeria’s kwenye penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya jumla ya magoli 2-2.

Kwa upande wa Al Ahly imecheza michezo 10 , imeshinda mechi sita , sare tatu  na kupoteza mchezo mmoja , magoli ya kufunga 19, huku magoli ya kufungwa yakiwa sita.

Kwenye hatua ya awali Al Ahly iliifunga timu ya AS Sonidep ya (Niger) kwa jumla ya magoli 5-0.

Al Ahly walikuwa kwenye kundi  (A) pamoja na  Simba (Tanzania), AS Vita (DR Congo) na El Merriekh (Sudan) na Al Ahly walimaliza kundi hilo wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 11, wakishinda michezo mitatu wakitoa sare katika michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.

Kwenye hatua ya robo fainali Al Ahly ilishinda kwa magoli 3-1 kwa ujumla dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Esperance ni mabingwa wa kombe hili mara nne huku mara ya mwisho wakilichukua  msimu wa Mwaka 2018-19.

Al Ahly ndio mabingwa wa kihistoria katika michuano hii ya Ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF) wakiwa wamechukua kombe hili mara tisa.

Al Ahly na  Esperance wamekutana kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika mara 18, ambapo Esperance imeshinda michezo minne, Al Ahly wakishinda michezo sita, huku michezo nane ikiisha kwa sare, Esperance ikifunga magoli 15 huku Al Ahly wakifunga magoli 18.