Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

18 kuiwakilisha Zanzibar Spice Boys Brazil

ZNZ Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Oktoba 10, 2026 hadi Oktoba 15, 2026, huko Minas Gerais nchini Brazil, huku kikosi hicho kikitarajiwa kuondoka Oktoba 5, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume, Zanzibar na kurejea Oktoba 18, 2026. Safari hiyo itashirikisha wachezaji, makocha na timu ya ufundi, Mkuu wa Msafara na maafisa wa Serikali ambapo Balozi Mstaafu Abdulsamad Abdulrahim anatarajiwa kuwa Mkuu wa Msafara.

KIKOSI cha vijana chipukizi cha Zanzibar Spice Boys, chenye wachezaji 18 wenye umri wa miaka 12 na 13, kinajiandaa kwenda Brazil kushiriki mashindano ya kimataifa ya soka la watoto yaliyopewa jina la PQ CUP BRASIL 2026.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Oktoba 10, 2026 hadi Oktoba 15, 2026, huko Minas Gerais nchini Brazil, huku kikosi hicho kikitarajiwa kuondoka Oktoba 5, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume, Zanzibar na kurejea Oktoba 18, 2026. Safari hiyo itashirikisha wachezaji, makocha na timu ya ufundi, Mkuu wa Msafara na maafisa wa Serikali ambapo Balozi Mstaafu Abdulsamad Abdulrahim anatarajiwa kuwa Mkuu wa Msafara.

Zanzibar Spice Boys imepangwa Kundi A la U-13, pamoja na Clube Minas Gerais, Soccer Pro Betim, Polo Novo Horizonte Rio Vermelho na Vitinho Soccer Itabira.

Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha timu kutoka Brazil, Ureno, Argentina na mataifa mengine, jambo litakalowapa vijana hao nafasi ya kupata uzoefu wa kimataifa na kupima uwezo wao dhidi ya vipaji mbalimbali.

Mkuu wa Msafara, Balozi Mstaafu Abdulsamad Abdulrahim, amesema safari hiyo inalenga zaidi ya ushindani wa uwanjani, ikiwemo kukuza vipaji, kujenga kujiamini, nidhamu pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimichezo na kitamaduni.

“Safai hii inalenga zaidi ya ushindani wa uwanjani, kwa kuwa inatoa fursa ya kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi, kuwajengea kujiamini, nidhamu pamoja na kupata uzoefu wa mazingira mapya ya soka.”€

 Naye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Riziki Pembe Juma, amesema ushiriki huo utawapa wachezaji nafasi ya kujifunza, kukuza vipaji na kupata uzoefu wa kimataifa na kuitangaza Zanzibar kimataifa.

“Ushiriki wenu utakuza vipaji vya watoto na kutangaza utamaduni na utalii wa Zanzibar Kiamtaifa, tunawatakia kila la kheri mkaipeperushe vyema bendera ya Tanzania,” amesema Pembe.