Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi, Kaze mtegoni Yanga

YANGA ipo Tunisia kwa ajikj ya marudiano la mtoano wa kuwania kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya, Club Africain, huku makocha Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze wakiingia mtegoni kulinda vibarua.

Timu hiyo ililazimishwa suluhu kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Kwa Mkapa Jumatano iliyopita na wiki ijayo italazimika kupata sare yoyote ya mabao au kushinda ili kutinga makundi kutuliza mashabiki waliopagawa baada ya kung’olewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Upepo haujawakalia vizuri makocha hao wa Yanga, kutokana na kuwepo kwa presha kubwa na kwamba kama timu hiyo itakosa matokeo mazuri katika mchezo huo ugenini basi ajira zao zinaweza kuishia hapo imefahamika.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga ni kwamba kabla ya mechi hiyo ya jijini Dar es Salaam mabosi wa klabu hiyo walikutana na makocha hao kisha kuwapa msimamo wao wakiwaambia kuwa, kama timu yao haitafuzu hatua ya makundi basi ndoa yao itaishia hapo hakuna namna.

Japo, Yanga mapema ilikanusha mpango wa kutaka kumtimua Nabi, lakini Mwanaspoti linafahamu kuwa hesabu hizo zilizuilika kwa muda tu, kwani ilishapanga kumpiga chini kutokana na mabosi wa klabu kutoridhishwiana mwenendo wa timu yao hasa kwenye anga la kimtaifa.

Lakini kwa sasa mabosi wa Yanga wanaona timu yao inazidi kuporomoka taratibu baada ya kubaini msuguano wa makocha hao ambao inaelezwa wamekuwa wakipishana kauli mara kwa mara unasabisha kuyumba kwa kikosi chao.

Tayari Kaze na bosi wake wanafahamu kwamba hatima ya ajira zao ko katika dakika 90 za ugenini na kwamba kabla ya kuondoka sio mbaya kwao kila mmoja akaweka vizuri mizigo yake tayari kwa ajili ya uamuzi wowote.

Mara baada ya mchezo huo mabosi wa Yanga walikutana na kufanya mazungumzo ambayo pia yaliendelea hadi juzi kabla timu haijaondoka wakiona hakuna haraka ya kuchukua maamuzi hayo kwa kusubiria kwanza mchezo wa marudiano ugenini ili kufanya maamuzi kwa afya ya timu hiyo.

“Unajua ni vile tumeshindwa kushinda, lakini suluhu sio mbaya ndio maana tumeona hakuna haja ya kuwoandoa sasa, licha ya hii presha kutoka kwa mashabiki ambao wanataka tuwaondoe, tunaangalia mbali kwa kuwa hii mechi haijaisha,” alisema mmoja wa vigogo wa juu wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa kwa jina lake gazetini.

Kocha Nabi ambaye jana Uwanja wa Ndege aliwashukuru mashabiki wanaomuunga mkono na wanaomkosoa, kana kwamba anawaaga, aliliambia Mwanaspoti, licha ya presha iliyopo kwao kama makocha, lakini bado wanao wajibu wa kuendelea na maandalizi ya kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa genini.

“Makocha siku zote tuko katika presha. Hii ni asili ya kazi yetu. Tunaendelea kuwajibika kuelekea mchezo wa marudiano, hatujakata tamaa,” alisema.