Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa yalia kuhujumiwa

WAKATI pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara likihitimishwa leo kwa timu zote kushuka uwanjani, Mtibwa Sugar itakayokuwa ugenini jijini Dar es Salaam imelia kuhujumiwa kabla ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania.

Mabosi wa klabu hiyo wamelia na Bodi ya Ligi (TPLB) kwa kuwabadilishia uwanja wakiwa tayari wapo mjini Iringa na kurudishwa Dar es Salaam, kitu walichodai ni kama wamehujumiwa.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mohammed Badru alisema wameshangazwa kuambiwa mechi haitachezwa tena mjini Iringa kwenye Uwanja wa Samora na badala yake wawahi Dar kuvaana na JKT Uwanja wa Azam Complex.

Badru alisema awali waliambiwa mchezo huo utapigwa Iringa kabla ya kubadilishiwa na kudai wamesikitishwa na badiliko hilo la ghafla bila ya kuwa naa taarifa mapema.

“Baada ya mchezo wetu na Dodoma Jiji tulienda Iringa tulipoelezwa mechi yetu na JKT Tanzania itachezwa Samora, ghafla tena tunaletewa taarifa za kuwa mchezo wetu utachezwa Chamazi wakati sisi tulishafika hapa Iringa, kwa hakika ni jambo la kusikitisha sana kwenye ligi yetu” alisema

Hata hivyo, Bodi ya Ligi ilitoa ufafanuzi kupitia Mtendaji Mkuu wake, Almas Kasongo aliyesema ni kweli ratiba ya mchezo huo ilibadilishwa na hii ni baada ya kupokea barua kutoka kwa uongozi wa JKT Tanzania na klabu zote mbili zilijulishwa kuhusu mabadiliko hayo.

“Kanuni zinaruhusu kwa timu mwenyeji kuchagua uwanja wa nyumbani na ni kweli mchezo huo ulipangwa kuchezwa Samora ila uongozi wa JKT waliletea barua kuomba mchezo wao uchezwe Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, Mbweni Dar es Salaam badala ya Samora ila sisi kama Bodi ya Ligi kwa kushirikiana na TFF tuliona uwanja huo sio rafiki na kuamua mchezo huo kuchezwa Azam Complex Chamazi na timu zote mbili zilipewa taarifa ya mabadiliko hayo” alisema Kasongo.

Timu hizi zinakutana katika mchezo wa mwisho wa Ligi huku kila timu ikipambania kuepuka janga la kushuka daraja, kwani JKT ipo nafasi ya 15 na pointi zao 36, huku Mtibwa ikiwa nafasi ya 13 na pointi 39 na kama kila moja itateleza inaweza kushuka ama kuangukia kwenye play-off.