Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF: Simba, Yanga tunaamsha Septemba 11

SIMBA na Yanga ambazo tayari zimefuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, zina muda usiozidi wiki tisa kuanzia sasa kabla ya kushuka uwanjani kwenye mechi zao za kwanza.

Kwa mujibu wa kalenda mpya ya Shirikirisho la Soka Barani Afrika(CAF) mechi za awali za mtoano zitapigwa wikiendi ya Septemba 10 na 12 na marudiano wiki moja baadae.

Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Biashara United na Azam nao ratiba yao itafuata utaratibu huohuo.

Lakini katika mpangilio huo wa Simba,Yanga haijaonyeshwa kwamba ni nani atakayeanzia ugenini au nyumbani mpaka ratiba rasmi itakapotoka mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi ujao.

Tanzania ndio nchi pekee ya Afrika Mashariki iliyopewa kwa maranyingine nafasi ya kuwakilishwa na timu nne kimataifa kutokana na ufanisi wa Simba msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambako waliishia robofainali.

Ratiba hiyo mpya ya CAF itapangiwa Jijini Cairo, Misri ambako Simba itakuwa ikiendelea na kambi yao ya mazoezi kujinoa na msimu mpya pamoja na kuweka mambo mengine sawa.

Kocha wa Simba, Didier Gomes na uongozi ndio walioikubaliana kambi kuwekwa jijini Cairo kutokana na hali ya hewa.

Lakini Mwanaspoti linajua kwamba Yanga wao wamepanga kuweka kambi yao nchini Uturuki kwenye visiwa vya Antalya ingawa bado kuna viongozi wanaopendekeza timu iende nchini Morocco. Nabi ambaye amependekeza kusajiliwa kwa wachezaji wapya nane wa kigeni msimu ujao, ameridhia kwenye nchi yoyote kati ya hizo lakini akipendelea zaidi Antalya.

Staa wa zamani wa Yanga, Simon Msuva anayekipiga kwenye klabu ya Waydad Casablanca ya Morocco yuko kwenye mawasiliano ya karibu na Jangwani wakimuuliza uwezekano wa kikosi hicho kuinjoi mazingira na miundombinu ya soka nchini humo.

Yanga imepania kurudi kwa nguvu kwenye michuano hiyo ya kimataifa, baada ya kuishia hatua ya makundi ya Shirikisho msimu wa 2018 na kuwa wa mwisho kundini walipokuwa wamepangwa wa USM ya Algeria, Rayon ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya.