Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Mzimbabwe wa Simba achimba mkwara

SAA chache tu tangu asainishwe mkataba wa kukipiga Msimbazi, beki mpya wa kati kutoka Zimbabwe, Peter Muduhwa amechimba mkwara kwa mabeki wa kati aliowakuta kikosini akiwamo Joash Onyango na Pascal Wawa akisema mkataba wake na mabingwa hao upo hai kwa mechi sita tu za Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini hesabu zake zikaenda mbali zaidi ya muda huo.

Muduhwa, ambaye ni beki wa timu ya taifa ya Zimbabwe aliyesajiliwa akitokea Fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (Chan) zinazoendelea nchini Cameroon, alisema kazi ambayo anataka kuifanya ndani ya klabu hiyo ndio itaamua atakuwapo kwa muda gani katika kikosi hicho.

Muduhwa alisema ameiona Simba na kwamba ni timu inayoundwa na wachezaji wengi bora hususan mabeki wenzake, lakini akasema wala hilo halimtishi anachotaka ni kupata nafasi.

Alisema hataki kuangalia amewakuta mabeki gani, lakini kupitia uwepo wa kocha mpya anataka kujipanga kila itakapokuja mechi ya Ligi ya Mabingwa awe sehemu ya kikosi cha kwanza.

“Simba ni timu kubwa nimeona wachezaji bora wengi ndani ya hii timu, nafikiri hii ni changamoto nzuri kwa kila mmoja kutakiwa kupambana na binafsi nipo tayari kwa hilo,” alisema Muduhwa.

“Hata mabeki niliowakuta ni wazuri na wanaonekana kuwa na uzoefu wa kutosha, nilipata maumivu ya kifundo cha mguu kule kwenye Chan lakini nikipona nataka kuhakikisha nakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza katika timu itakayocheza mechi za Ligi ya Mabingwa.

“Jambo zuri hapa kuna kocha mpya ambaye amefika kitu muhimu ni kuonyesha ubora wako ili aweze kukuamini nafahamu haitakuwa rahisi, lakini nataka hilo litimie ili niweze kubaki zaidi hapa Simba.”

Kwa sasa ukuta wa Simba una majembe kama Onyango, Wawa, Kennedy Juma na Ibrahim Ame ambao wameisaidia timu hiyo kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikipangwa Kundi A pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita ya DR Congo na El Merreikh ya Sudan.