Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yes! Samia na michezo damdamu

RAIS Pict

Muktasari:

  • Kama hujui imetimia miaka minne tangu Rais aapishwe rasmi kuwa Rais wa Tanzania akirithi nafasi ya John Magufuli ‘JPM’ aliyefariki kutokana na ugonjwa wa moyo.

UTASEMA nini kuhusu michezo hususani soka, bila kulitaja jina la Sais Samia Suluhu Hassan.

Kama hujui imetimia miaka minne tangu Rais aapishwe rasmi kuwa Rais wa Tanzania akirithi nafasi ya John Magufuli ‘JPM’ aliyefariki kutokana na ugonjwa wa moyo.

Ndani ya miaka minne, Rais Samia amejipambanua kuwa, mdau mkubwa wa sekta ya michezo kwa ushiriki wake katika shughuli mbalimbali za sekta hiyo pamoja na mipango iliyowekwa na uongozi wake wa kuhakikisha michezo inapiga hatua na sasa kila kitu kimeonekana kwa vitendo na si maneno.

Ushiriki huo wa Rais Samia katika michezo umeonekana kujenga imani ya wengi kuwa huenda sekta ya michezo ikapata mafanikio makubwa chini ya utawala huo kama imani ilivyo katika sekta nyingine.

Ipo mifano na uthibitisho wa wazi unaoonyesha jinsi Rais Samia anavyotamani kuona michezo sio tu inakuwepo kwa ajili ya kujifurahisha bali kugeuka fursa ya ajira na kukuza uchumi wa nchi.

Wakati huu kila mmoja anazungumza fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani  (CHAN) zinazoanza leo, Agosti 2, 2025 zikiandaliwa kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, tambua bila nguvu ya Rais Samia ilikuwa ngumu Tanzania kupewa nafasi hii. Kuandaa CHAN kunahitaji mambo mengi zaidi ya kuwa tu na timu ya taifa na Rais Samia alisimama katikati sambamba na Rais wa Kenya, William Ruto na wa Uganda, Yoweri Museveni na kuitangazia dunia kuwa Tanzania ipo tayari kuandaa mashindano hayo na yale Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

RA 01

Na kauli hiyo kwa sasa inaonekana kwa vitendo ikiwa leo Agosti 2, 2025 ndio siku ya ufunguzi wa michuano ya nane utakaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam.

CHAN ni mashindano ya pili kwa ukubwa Afrika baada ya ile ya AFCON, hivyo kitendo cha Rais Samia kujitokeza hadharani na kukubali, nchi itaandaa michuano hii ni jambo kubwa na la kishujaa ambalo kila mmoja anatakiwa kuliongeza.

Kuna faida nyingi ambazo zinapatikana kabla na baada ya mashindano hayo, ambayo moja kwa moja yanawagusa Watanzania, hivyo alichokifanya Rais Samia ni kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Kwa ujumla, kuwa mwenyeji wa mashindano ya CHAN ni zaidi ya mchezo ni fursa ya kiuchumi, kijamii na kimataifa inayoweza kuleta mabadiliko chanya ya muda mrefu kwa Tanzania.

Fedha za serikali zimetumika kwa sehemu kubwa katika ukarabati na ujenzi wa viwanja vya kisasa, vituo vya mazoezi na miundombinu mingine ya michezo.

Hii inaonyesha kuwa, Rais Samia amesaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha mazingira ya michezo nchini kwa muda mrefu hata baada ya mashindano kumalizika.

Jambo lingine amesaidia fursa za kiuchumi na kibiashara, wakati wa mashindano, wageni (wachezaji, maofisa, mashabiki) wataongeza matumizi ya huduma mbalimbali kama hoteli, usafiri, chakula na burudani, jambo linalosaidia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Wafanyabiashara wadogowadogo nao ni kati ya wale ambao wanapata faida ya mashindano haya.

Pia ni ni fursa bora ya Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia matangazo ya mashindano na wageni wanaokuja kushuhudia mechi, pamoja na wale ambao watatazama kupitia vituo vikubwa vya televisheni ambavyo vitaonyesha mashindano hayo na kuongeza watalii watakaokuja kutembelea vivutio kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro, na Zanzibar kabla au baada ya mashindano.

RA 02

SAMIA NA STARS

Rais Samia amejipambanua kuwa mwanamichezo hodari kiongozi anayetaka kuona timu ya taifa, Taifa Stars inafanya vizuri na kupata mafanikio, mwaka jana aliongoza harambee maalum ya kuzichangia timu za taifa za michezo mbalimbali ili kuziwezesha kuwa na ushiriki mzuri katika mashindano ya kimataifa.

Katika harambee hiyo iliyosimamiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kilipatikana kiasi cha fedha Sh3.7 bilioni. Huu ni uzalendo wa kutosha kuonyesha kuwa, Rais Samia amekuwa akionyesha kwa vitendo.

Pia hivi karibuni kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi alitangaza Rais Samia ametoa ahadi ya Sh1 bilioni kwa Stars ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

“Katika kuchagiza hamasa kwa timu yetu ya taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya donge nono la fedha za Kitanzania Shilingi 1 Bilioni kwa vijana wetu wa Taifa Stars iwapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano haya ya CHAN 2024,” alikakariwa Profesa Kabudi wakati akitoa taarifa hiyo kwa umma wiki iliyopita.

RA 03

UJENZI, UKARABATI VIWANJA

Wakati utawala wa Rais Samia unaingia madarakani, uliahidi utatenga bajeti ya fedha kwa ajili ya kusaidia maboresho ya viwanja kadhaa vya soka vilivyoonekana kuwa na uchakavu na tayari hilo limeshaanza kuonekana kwa vitendo kwa viwanja kadhaa kufanyiwa maboresho na vingine kujengwa upya.

Kana kwamba haitoshi, uongozi wa Rais Samia umeahidi ujenzi wa viwanja viwili vya kisasa vya soka katika miji ya Dodoma na Arusha vilivyoanza ujenzi wake vikitarajiwa kutumika katika fainali za Afcon 2027.

“Kwa kasi hii ninayoiona, Watanzania wana uhakika wa kuandaa AFCON 2027, napenda kumpongeza mkandarasi kwa jinsi anavyofanya kazi yake, hii ni kazi nzuri na sasa tunaelekea sehemu nzuri sana, kabla ya muda uliopangwa uwanja huu utakuwa umeshakamilika,” alisema Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ alipotembelea ujenzi wa uwanja Arusha

Uwanja wa Benjamin Mkapa mara kadhaa umekuwa ukifungwa ili kufanyiwa ukarabati lengo ni kuufanya uwe bora zaidi ili fainali za Afcon 2027, zitakapokuja uwe katika hali nzuri na wenye kukidhi viwango, lakini pia kumbuka wakati wa maandalizi haya ya CHAN, serikali ilitumia kiasi cha Sh31 bilioni, hizi ni fedha ambazo serikali imetoa ili kuhakikisha kuwa mashindano haya yanakuwa bora, na picha ya uwanja inaonyesha uhalisia wenyewe.

RA 04

AFCON 2027

Uongozi wa Rais Samia ulianzisha wazo la kuomba kuandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2027 ambapo baada ya kufanyika ushauri wa kitaalamu, ilionekana ingekuwa jambo gumu kwa Tanzania kuandaa yenyewe fainali hizo kutokana na kutokuwa na viwanja vya kutosha lakini changamoto ya kibajeti.

Kutokana na hilo, ilishauriwa kwamba ni vyema Tanzania ingeomba kuandaa kwa pamoja mashindano hayo na nchi za Kenya na Uganda ambazo ipo nazo pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini pia ni wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati CECAFA).

Rais Samia kwa nafasi yake alifanikiwa kuwashawishi Rais wa Kenya, William Ruto na wa Uganda, Yoweri Museveni ambao waliridhia wazo la kuandaa kwa pamoja mashindano hayo na kuwaagiza mawaziri wa michezo wa nchi zao, kukutana ili kuandaa mkakati wa kuhakikisha maombi ya kuandaa fainali hizo yaliyopewa jina la ‘Pamoja Bid’ yanapata ushindi katika kinyang’anyiro hicho. Katika kuyapa nguvu maombi hayo, Rais Samia, Museveni na Ruto kila mmoja aliahidi serikali yake kuchangia kiasi cha Dola 30 milioni (Sh76.7 bilioni) kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya fainali hizo. Ndoto hizo za Rais Samia, zilitimia rasmi Septemba 27, 2024 baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk Patrice Motsepe kutangaza maombi hayo ya pamoja ya Tanzania, Kenya na Uganda yameshinda kuandaa Afcon 2027 yakiibuka kidedea mbele ya Botswana, Algeria, Misri na Senegal.

RA 05

GOLI LA MAMA

Utawala wa Rais Samia mwaka 2022, ulianzisha utaratibu wa kuzipa hamasa klabu za Tanzania zilizokuwa zinashiriki mashindano ya Afrika likipewa jina kama ‘Bao la Mama’ kwa kutoa kiasi cha Sh5 milioni kwa kila bao ambalo timu hizo zilikuwa zinafunga kuanzia makundi huku hatua za mbele dau hilo likiongezeka.

Hamasa hiyo ya fedha za ‘Bao la Mama’ ambazo Rais Samia alikuwa anatoa ilichangia kwa kiasi kikubwa kuzipa morali Simba na Yanga, ambazo zilijitutumua na kufika hatua za juu za mashin-dano hayo, kumbuka katika utawala wa Rais Samia ndio timu zote zimekuwa na mafanikio makubwa zaidi kwa soka, Yanga ikifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022-2023 sawa na Simba 2024-2025. Lakini katika kipindi hiki cha Rais Samia, kutokana na sapoti ambayo amekuwa akiitoa kwenye timu  imeonekana kuleta chachu, ambapo Tanzania imeandika historia ya kuingiza kwa mara ya kwanza timu mbili kwa mpigo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu mmoja nyuma. Lakini hamasa hiyo ya fedha haijaishia kwa klabu tu bali hata timu ya taifa imeonja ladha ya fedha za Rais Samia baada ya kufuzu fainali za AFCON zilizofanyika mwaka jana huko Ivory Coast.

Rais Samia aliahidi kama Taifa Stars itafuzu AFCON, angetoa bonasi ya Sh500 milioni, fedha ambazo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikabidhi hundi yake, Oktoba 3, 2023.

Mbali na fedha hizo, serikali ya Rais Samia pia iliahidi kununua kila bao la Taifa Stars katika mechi za kufuzu na zile za Afcon kwa dau la Sh10 milioni, hayo ni mambo ambayo yanaonyesha kuwa Rais Samia amefanya kazi yake kwa vitendo na kuonyesha jinsi ambavyo anataka kuona soka linapiga hatua hapa nchini.


SOKA LA WANAWAKE CECAFA

Agosti 21, 2021, Rais Samia alikubali ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la kuwa mdhamini wa Mashindano ya Wanawake ya Cecafa.

Rais Samia alibainisha hayo Ikulu, Dar es Salaam wakati wa hafla ya chakula cha mchana na wachezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 23 na ile ya riadha ya Olimpiki. “Rais wa TFF, Wallace Karia, aliniambia mpango wao wa kutaka kuanzisha Cecafa Woman Championship kila mwaka.

“Amenipa mfano wa Rwanda, rais wao Kagame anadhamini mashindano akaniomba na mimi nidhamini haya, nilimuuliza ni kiasi gani ili nipime misuli yangu.

“Aliponipa bajeti na kupima misuli yangu niliona mwenyewe siwezi, sitoweza lakini nitajua nitakapozipata pesa hizo, hivyo nawaambia nitadhamini haya mashindano,” alisema Rais Samia wakati akitangaza kuridhia ombi hilo.

Kwa mujibu wa Rais wa TFF, Karia udhamini huo utakuwa ni kwenye mashindano ya timu za taifa za wakubwa za wanawake za nchi wanachama wa Cecafa, jambo ambalo limekuwa endelevu na kuzifanya timu za soka za wanawake kupiga hatua kwa kiasi kikubwa, hali ambayo imeifanya hata Twiga Stars kufuzu kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wanawake (WAFCON).