Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Washambuliaji wanavyozibeba timu Ligi Kuu

Washambuliaji Pict

Muktasari:

Hadi wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inatangaza kusimama kwa ligi hiyo, Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 40 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 39 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.

Ligi Kuu ya NBC imesimama kwa muda wa miezi miwili ili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika kisiwani Pemba na pia kupisha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ligi za ndani (CHAN), ambazo Tanzania ni moja ya wenyeji, nyingine zikiwa ni Kenya na Uganda.

Hadi wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inatangaza kusimama kwa ligi hiyo, Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 40 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 39 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.

Mkiani mwa msimamo wa ligi ipo KenGold yenye pointi sita, Kagera Sugar ikishika nafasi ya 15 na pointi zake 11 huku Pamba Jiji FC yenye pointi 12 ikiwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Idadi ya mabao 266 tayari yameshafungwa kuanzia pale msimu ulipoanza hadi sasa wakati ligi inasimama huku timu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi ikiwa Yanga ambayo ina mabao 32 na zilizofunga mabao machache zaidi zikiwa ni Tanzania Prisons na Pamba Jiji ambazo kila moja imefunga mabao saba.

Ni msimu ambao unaonekana kuanza vyema kwa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji kwabni ndio wametoa mchango mkubwa katika kupatikana kwa mabao ya timu zao kulinganisha na wachezaji wa nafasi zingine.

Ifuatayo ni tathmini ya jinsi washambuliaji walivyotimiza vyema jukumu lao kuanzia mwanzoni mwa msimu hadi sasa ligi iliposimama.


SIMBA

Simba imefunga mabao 31 katika mechi 15 ambapo kati ya hayo, 13 yamefungwa na washambuliaji na mengine 13 yamepachikwa na viungo huku mabeki wakifunga mabao matano.


YANGA

Idadi kubwa ya mabao ya Yanga yamepachikwa na washambuliaji ambapo kati ya 32 iliyopata kwenye ligi msimu huu, 14 yamewekwa kimiani na wachezaji wa nafasi hiyo, 13 yakifungwa na viungo na manne ya mabeki huku ikiwa na bao moja la kujifunga la timu pinzani.


AZAM

Azam FC inashika nafasi ya tatu kwa kufunga mabao mengi ikiwa nayo 25 ambapo kati ya hayo, mabao 15 yamepachikwa na washambuliaji.


Katika hali ya kushangaza, mabeki wa Azam FC wamefunga idadi kubwa ya mabao kuliko viungo wao ambapo wamefumania nyavu mara sita huku viungo wakifunga manne.


FOUNTAIN GATE

Katika mechi 16 ambazo imecheza kwenye ligi msimu huu, Fountain Gate imefumania nyavu mara 24 ambapo mabao 19 yamepachikwa na washambuliaji na yaliyobakia matano yakifungwa na viungo.


SINGIDA BLACK STARS

Idadi kubwa ya mabao ya Singida Black Stars imepachikwa na viungo ambayo ni 11, washambuliaji wakifumania nyavu mara nane na mabao matatu yamefungwa na mabeki.


TABORA UNITED

Mabao 19 yamefungwa na Tabora United katika mechi 15 za Ligi msimu huu ambapo kati ya hayo, mabao 11 ni ya washambuliaji, viungo wamefunga mabao sita na mabeki wamepachika mabao mawili.


DODOMA JIJI

Dodoma Jiji imefunga mabao 16 katika Ligi msimu huu na kazi kubwa inaonekana kufanywa na washambuliaji ambao wamefunga mabao 11, mabeki wakifunga mabao manne na moja likiwa la kiungo.


COASTAL UNION

Kama ilivyo kwa Dodoma Jiji, Coastal Union nayo imefunga mabao 16 ambapo mabao 13 yamefungwa na washambuliaji, mawili yakifungwa na beki na bao moja ni la kiungo.


MASHUJAA FC

Maafande wa Mashujaa FC wamefumania nyavu mara 14 katika Ligi Kuu hadi sasa. Mabao 13 yamefungwa na washambuliaji na bao moja limepachikwa na kiungo.


KMC

Timu ya KMC imefunga mabao 11 kwenye mechi 16 ambazo imeshacheza kabla ya Ligi kusimama ambapo kati ya mabao hayo 11, mabao saba ni ya washambuliaji, moja ni la kiungo na matatu ya mabeki.


NAMUNGO

Mabao 11 yamefungwa na Namungo FC msimu huu, washambuliaji wamefunga mabao manne, viungo mabao matano na beki amefunga mabao mawili.


KENGOLD

Mabao 10 kati ya 11 ya KenGold kwenye Ligi Kuu msimu huu yamefungwa na washambuliaji huku moja tu likifungwa na kiungo.


KAGERA SUGAR

Kagera Sugar imebebwa na washambuliaji hadi sasa ambapo wamefunga mabao saba kati ya 10 ambayo timu hiyo inayo, vingo wakifunga mabao mawili na moja ni la beki.


JKT TANZANIA

Maafande wa JKT Tanzania wamefumania nyavu mara 10 katika mechi 16 za Ligi Kuu msimu huu. Mabao sita ni ya washambuliaji, matatu ya viungo na moja la beki.


TANZANIA PRISONS

Mabao saba tu yamefungwa na Tanzania Prisons kwenye Ligi Kuu msimu huu. Vinara wa ufungaji kwenye kikosi chao ni viungo waliofunga mabao matatu sawa na mabeki huku bao moja tu likipachikwa na mshambuliaji.


PAMBA

Pamba imefunga mabao saba ambapo washambuliaji wamefunga mabao matano, viungo mabao mawili na bao moja limefungwa na beki.