Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WAPEWE, WASIPEWE? Arsenal itakavyoitibulia Liverpool ubingwa

UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Anfield inayonolewa na Mdachi Arne Slot imepanua pengo hilo la pointi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United, wakati wapinzani wao walioaminika kwamba watasumbua kwenye mbio za ubingwa, Arsenal ilibanwa ugenini City Ground kwa kutoka 0-0 na Nottingham Forest.

LONDON, ENGLAND: LIVERPOOL imetanua mbawa zake kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuweka pengo la pointi 13 dhidi ya timu inayoshika namba mbili, ambao ni Arsenal ya kocha Mikel Arteta.

Miamba hiyo ya Anfield inayonolewa na Mdachi Arne Slot imepanua pengo hilo la pointi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United, wakati wapinzani wao walioaminika kwamba watasumbua kwenye mbio za ubingwa, Arsenal ilibanwa ugenini City Ground kwa kutoka 0-0 na Nottingham Forest.

Kinachoelezwa, Liverpool mechi zake ngumu zilizokuwa zikitia mashaka kwamba watafanya hovyo, zimeshakwisha. Kipindi hicho kigumu, Liverpool ilicheza mechi tano za Ligi Kuu England ndani ya siku 15, zote dhidi ya wapinzani wagumu, na haikupoteza mchezo wowote. 

Sambamba na hilo, ilipata ushindi dhidi ya wapinzani ambao itakutana nao kwenye fainali ya Kombe la Ligi, Newcastle United na imewachapa mabingwa watetezi, Manchester City na kupenya mbele ya Wolves ya mkali Matheus Cunha katika harakati zao za kuhakikisha wanabaki kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Ugenini kwa wapinzani wao Everton - mechi yao ya mwisho ya Merseyside derby uwanjani Goodison Park - na ile ya wagumu Aston Villa ambazo ziliaminika zitakuwa na ugumu kwa Liverpool, zote hizo ilitoka sare ya mabao 2-2.

UBIN 01

MEZA INAWEZA KUPINDUKA?

Ni mara moja tu kwenye historia ya Ligi Kuu England kwamba ilitokea timu iliyokuwa imeachwa nyuma kwa pointi 13 ilipindua meza na kwenda kubeba ubingwa wa ligi hiyo. Na kinachovutia, timu hiyo ni Arsenal, ilipofanya hivyo katika msimu wa 1997/98.

Hata hivyo, kwa wakati huo Arsenal ilikuwa na mechi 19 bado, ilipopindua meza mbele ya Manchester United na kubeba taji hilo la Ligi Kuu England ikiwa chini ya kocha Arsene Wenger. Lakini, kipindi hiki ikiwa chini ya Mikel Arteta, imebakiza mechi 11 tu.

Itaweza? Kama Arsenal itaweza kupindua meza na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England wakati huu ikiwa imeachwa pointi 13 na ina mechi 11 tu za kucheza, basi pengine huo utakuwa ubingwa wa kihistoria zaidi katika mikikimikiki hiyo.

UBIN 02

LIVERPOOL ITABEBA UBINGWA LINI?

Kutokana na kuhitajika kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Ligi, itakayopigwa Machi 16, kisha itafuatia mapumziko ya mechi za kimataifa kwa mwezi huo Machi, Liverpool itacheza mechi moja tu ya Ligi Kuu England ndani ya mwezi huu - itakapokwaana Southampton - hivyo, ikishinda, inaweza kutangaza ubingwa mapema tu mwezi ujao.

Ukweli ni kwamba, kama matokeo yatakuwa mazuri upande wao, basi mapema ambayo Liverpool inaweza kutangaza kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, inaweza kuwa wikiendi ya Aprili 5/6, ambapo itakuwa na pointi 78 wakati inaifuata Fulham. Lakini, ili hilo litokee, basi itahitaji kushinda mechi zao zota tatu zijazo, ikiwamo ile ya Craven Cottage, huku Arsenal ikutwe na majanga ya kupoteza mechi nne zijazo.

Nottingham Forest, ambayo inaweza kukusanya pointi hadi 81, Man City (80) na Chelsea (79) nazo zinapaswa kuangusha pointi kabla ya kufika muda huo.

Kama Liverpool itaendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 13, basi wanaweza kuthibitishwa kuwa ni mabingwa wa Ligi Kuu England katika wikiendi ya Aprili 26/27, wakati itakapocheza Anfield dhidi ya Tottenham Hotspur, ambapo hapo itakuwa imebakiza mechi nne tu kwenye Ligi Kuu England.

Kama pengo hilo la pointi la Liverpool litapungua hadi pointi 10, miamba hiyo ya Anfield itasubirishwa kubeba taji hilo hadi kwenye mwezi wa mwisho wa msimu huu, ambapo inaweza kushinda itakapokwenda ugenini kucheza na Chelsea wikiendi ya Mei 3/4.

Liverpool itakuwa nyumbani kucheza na Arsenal wikiendi inayofuatia, Mei 10/11, ambapo hapo itakuwa imebakiza mechi mbili tu kumaliza msimu.

Kama hadi muda huo, kikosi hicho cha Slot kitakuwa kinaongoza kwa tofauti ya pointi saba kileleni, sare au ushindi utatosha kuwafanya kuwa mabingwa wa taji hilo mbele ya Arsenal - ambao kama watakuwa wataendelea kupambana kwenye mbio.

UBIN 05

                  

TIMU GANI ILIBEBA UBINGWA MAPEMA?

Kuna vipimo viwili vya kutambua timu iliyobeba ubingwa mapema kwenye msimu - ile ya kalenda ya mwaka na nyingine ni ya kuhusu idadi ya mechi ilizocheza.

Liverpool inashikilia rekodi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa imecheza mechi chache, wakati iliponyakua taji hilo baada ya mechi 31 katika msimu wa 2019/20.

Kitu kingine ilichoweka rekodi Liverpool kwenye ubingwa wao uliopita kwamba msimu ulisogezwa mbele kutoka Machi hadi Juni kutokana na janga la Uviko - 19; ambapo miamba hiyo ilitangazwa kuwa mabingwa, Juni 25, 2020.

Manchester United hivyo bado inashikilia rekodi ya kubeba ubingwa wa haraka zaidi kwa mujibu wa kalenga, ilipofanya hivyo msimu wa 2000/01, ambapo ilithibitishwa kuwa mabingwa, Aprili 14, 2001.

Kuvunja rekodi yao wenyewe ya ubingwa kwenye mechi 31, Liverpool itahitaji kufanya maajabu, kuhakikisha kwamba wakati inakwenda kumenyana na Fulham, wikiendi ya Aprili 5/6, kwenye mechi yao ya 30, itangaza ubingwa hao.

Kama inataka kulinganisha na rekodi ya ubingwa uliopita, basi Liverpool inapaswa kunyakua taji hilo, wikiendi ya Aprili 12/13, ambapo itakipiga na West Ham United.

Kama hilo likitokea, basi Liverpool itakuwa imevunja rekodi ya Man United ya kubeba ubingwa wa ligi mapema kwenye kalenda.

UBIN 03

ARSENAL IFANYE NINI KUISHIKA LIVERPOOL?

Wakati Arsenal ikiwa nyuma kwa pointi 13 na Liverpool, bado ina mechi moja mkononi. Kama itashinda kiporo chake hicho, dhidi ya Chelsea, Machi 16, itafanya pengo la pointi kupungua na kubaki 10, lakini hiyo linategemea na matokeo ya mechi zijazo, ambapo Liverpool itakuwa Anfield kucheza na Southampton na Arsenal itakwenda Old Trafford kukipiga na Man Utd.

Kitu ambacho Arsenal inaomba kwa sasa Liverpool ipoteze au itoke sare, kwenye mechi hiyo, huku wao wakishinda ili kufanya pengo la pointi lisiwe zaidi ya tisa wakati watakapokutana wenyewe kwenye wikiendi ya Mei 10/11.

Kama Arsenal itashinda kwenye mechi hiyo ya Anfield kwa mara ya kwanza tangu Septemba 2012 - mechi ambayo Arteta anaweza kuwa na huduma ya mastaa wake, Bukayo Saka na Gabriel Martinelli. Na hilo likitokea, basi Arsenal inaweza kwenda kupindua meza kwenye mechi mbili zilizobaki kumaliza msimu, huku mpango ukiwa ni uleule tu kuomba mabaya kwa Liverpool.

UBIN 04

POINTI NYINGI KUPINDULIWA

Ni pointi nyingi kiasi gani ziliwahi kupinduliwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kihistoria? Ni swali linalovutia.

Ukweli ni kwamba hakuna timu iliyowahi kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 13 hadi kufikia sasa ulipofika msimu, kisha ikapinduliwa na kukosa ubingwa. Lakini, tofauti ya pointi 13 kama pointi, ziliwahi kupinduliwa katika msimu wa 1997/98, wakati Arsenal ya Arsene Wenger ilipoifanyia balaa Man United.

Man United ilikuwa na pointi nyingi hivyo hadi mwishoni mwa Desemba, na ilikuwa bado inaongoza kwa pointi ya pointi 12 dhidi ya Arsenal hadi kufikia Februari. Lakini, Arsenal ilifanya maajabu katika mechi zake 10 zilizofuata, ambapo ilishinda mfululizo, ambapo mechi ya pili kati ya hizo ilikuwa ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Man United uwanjani Old Trafford - na ilikuwa kutangaza ubingwa Mei 3 ikiwa na mechi mbili mkononi. Safari hii itawezekana?

Kwenye hesabu, hakuna ambacho hakiwezekani. Kama Arsenal itashinda kiporo chake, itafanya pengo la pointi kuwa 10.

Pengo la pointi 10 au zaidi, limeshawahi kupinduliwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England mara saba tofauti; ikiwamo pointi 13 ilizopindua Arsenal, pointi 12 ilizopindua Man United 1992/93 (dhidi ya Norwich City) na msimu wa 1995/96 (dhidi ya Newcastle) na pointi 10 zilizopindua Man United msimu wa 1996/97 (dhidi ya Liverpool), 2002/03 (Arsenal) na 2008/09 (Liverpool) na Man City in 2018/19 (Liverpool).

Kwa maana hiyo, Liverpool ilipoteza ubingwa wa Ligi Kuu England mara tatu kwa kupinduliwa licha ya kuongoza kwa tofauti ya pointi 10+. Je, Arsenal itawafanya vibaya na kuwa mara ya nne? Ngoja tuone.