Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchaguzi Yanga: Munir na Khimji wafunguka dira zao

Muktasari:

  • Upande wa rais na makamu wake tumemaliza, sasa ni kwa wajumbe ambapo leo tunaendelea kwa wagombea wengine wanaoitaka nafasi hiyo, Munir Said na Saady Khimji.

TUNAENDELEA kumulika Uchaguzi Mkuu wa Yanga, tukiangalia wasifu mbalimbali wa wagombea wa nafasi mbili za urais, makamu wake na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao wataingia kuwania nafasi saba za kuingia kwenye uongozi wa klabu hiyo.

Upande wa rais na makamu wake tumemaliza, sasa ni kwa wajumbe ambapo leo tunaendelea kwa wagombea wengine wanaoitaka nafasi hiyo, Munir Said na Saady Khimji.

Tuanze na Munir ambaye alikuwa kwenye kamati inayomaliza muda wake, akitaka tena nafasi hiyo kuendelea kuwa sehemu ya uongozi wa juu akiona bado anahitaji muda zaidi kuipa mafanikio klabu hiyo kongwe zaidi nchini.

Munir ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki makampuni mbalimbali yakiwemo Marania Group, alikuwa sehemu ya uongozi wa Yanga baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa mwaka 2022 akiwa mmoja wa wajumbe watano wa kuchaguliwa.

Ndani ya miaka minne, Munir sio mtu ambaye ungezoea kumuona sana akiongea kwenye vyombo vya habari lakini amekuwa akisifika kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye uamuzi wa kibiashara ndani ya klabu hiyo. Kigogo huyo amekuwa karibu sana na matawi tofauti ya wanachama wa klabu hiyo kwenye kuhamasisha kuwa sehemu ya kushiriki hatua za kimaendeleo, likiwemo suala la kujisajili na kuwa wanachama hai wa Wananchi.

Ukiwauliza mashabiki wa Yanga watakwambia Munir alikuwa mmoja ya watu waliosisitiza Yanga kusimama imara kwenye msimamo wa ile mechi ya Hatuchezi dhidi ya Simba, akipinga mambo ambayo hayapaswi kupewa nguvu kwenye ustawi wa soka.

Munir anataka kuendelea kuwa kiongozi wa Yanga akijivunia namna uongozi wao chini ya Rais Hersi Said ulivyokuwa na mafanikio lakini pia utulivu akisema malengo makubwa ni kuendeleza mafanikio waliyopata na kusimamia ukamilishwaji wa ujenzi wa uwanja ambao anaamini utajengwa kwa wakati uliopangwa na mfadhili wao Ghalib Said Mohammed.

“Mambo makubwa yamefanyika ndani ya muhula wa kwanza wa uongozi wetu lakini bado naona kuna nafasi ya kuwatumikia zaidi Wanayanga wenzangu, tuna kazi hazijamalizika hapa ndio maana tunarudi tena kwa waliotuchagua tukiwaomba ridhaa nyingine ili klabu yetu isogee kimafanikio, kuna mambo mengi unaona suala la uwanja, wapo wana wasiwasi, mimi nawatoa wasiwasi uwanja utajengwa,”€  anasema Munir.


KHIMJI ANATAKA KURUDI

Jina la Saad Khimji sio geni ndani ya wadau wa Yanga, jamaa amerudi tena akiutaka ujumbe baada ya kushika nafasi hiyo miaka ya nyuma.

Khimji aliwahi kuitumikia Yanga kwenye nafasi hiyo ya ujumbe kuanzia 2019 hadi 2022 wakati wa utawala wa aliyekuwa Mwenyekiti, Dk Mshindo Msola.

Dk Msola alimkabidhi Khimji kuongoza kamati ya matawi, wanachama, habari na hamasa kuanzia mwaka 2020 hadi 2022.

Khimji ndani ya jiji la Dar es Salaam ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Soka Mkoa huo (DRFA), akiwa pia ni mwenyekiti wa klabu ya Eleven Fighter. Kigogo huyu nje ya soka ni mwanasiasa Dar es Salaam akiwa diwani wa Kata ya Ilala ambayo ndani yake Yanga imo, kuanzia mwaka 2015 nafasi ambayo anaitumikia mpaka sasa ambapo pia amewahi kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala kuanzia mwaka 2020 hadi 2021.

Ukiacha uongozi huo, Khimji kitaaluma ni kocha wa mpira mwenye leseni daraja C aliyoamua kuisomea kutokana na mapenzi yake ya soka lakini hataki kufundisha timu kama makocha wengine bali ni kuwa na ujuzi. Licha ya Khimji kuwa nje kwa muda wa miaka mine, hakuwa mbali sana na mechi za timu hiyo, bado alikuwa sehemu ya watu wanaoifuatilia timu hiyo kwa karibu na kuwa na mawasiliano na viongozi waliokuwa madarakani.

Khimji anataka kurudi kutumikia nafasi hiyo huku akitangulia kuwapongeza viongozi wanaomaliza muda wao kuwa wamefanya kazi nzuri akitaka kuungana nao kuipa mafanikio Zaidi klabu hiyo.

“Watu wananiuliza kwanini narudi tena, kwasasa jibu ni moja tu, hii ni klabu ambayo wakati wote natamani kuwe na akili yangu kwenye kila hatua ya maendeleo, niwapongeze sana viongozi ambao wamemaliza miaka hii minnne wamefanya kazi kubwa sana,”€anasema Khimji.

“Uongozi ni kushirikiana na mimi nimeona nirudi kutafuta nafasi ya kuungana na wenzangu tutakaoshinda ili tuweze kuipa mafanikio zaidi klabu yetu, nipo kwenye serikali ya jiji nitashirikiana na wenzangu kuharakisha mambo kwenye kiu ya ujenzi wa uwa nja wetu.”