Prime
Walikuwa 'bize' na namba sita na kusahau kujiandaa
WIKIENDI iliyopita watani wa jadi wa Tanzania, Simba na Yanga, walikuwa na heka heka za matamasha yao ambayo sasa yamekuwa utamaduni.
Jumamosi ya Agosti 8, ilikuwa Simba Day na wenyewe waliitumia siku yao kuadhimisha miaka 90 ya uhai wao, huku Jumapili ya Agosti 9 ikawa zamu ya pacha wao, Yanga, wakisherehekea Siku ya Mwananchi.
Kama ilivyo kawaida, siku hizi huambatana na mechi na safari ilikuwa hivyo pia, lakini tofauti na miaka yote, kwa mara ya kwanza timu zote mbili zikajikuta zinapoteza mechi hizi.
iSimba alipoteza 1-0 kwa Polisi Kenya kabla ya Yanga kufungwa 2-1 na Les Aigle du Congo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tangu timu hizi zianze kusherehekea kwa pamoja matamasha haya mwaka 2019, haijawahi kutokea wote wakapoteza mechi zao...zaidi ya mwaka huu, 2026.
MATOKEO YA MUDA WOTE WA MATAMASHA
2019
Yanga 1-1 Kariobangi Sharks (Kenya)
Simba 3-1 Power Dynamos (Zambia)
2020
Yanga 2-2 Aigle Noir (Burundi).
Simba 6-0 Vital’o (Burundi)
2021
Yanga 1-2 Zanaco FC (Zambia)
Simba SC 0–1 TP Mazembe (DRC)
2022
Yanga SC 0-2 Vipers SC (Uganda)
Simba 2-0 St. George SC (Ethiopia)
2023
Yanga 1-0 Kaizer Chiefs (Afrika Kusini)
Simba 2- 0 Power Dynamos FC (Zambia)
2024
Yanga 2-1 Red Arrows FC (Zambia)
Simba 2-0 APR FC(Rwanda)
2025
Yanga SC 1-0 Bandari FC (Kenya).
Simba 2-0 Gor Mahia FC (Kenya)
2026
Yanga 1-2 Les Aigle du Congo (DRC)
Simba SC 0-1 Kenya Police FC (Kenya)
SABABU NI NAMBA SITA
Kuelekea matamasha haya timu zote mbili zilikuwa 'bize' kuinadi namba sita na kusahau kujiandaa vizuri. Sio mashabiki, sio viongozi, kila mmoja alikuwa akiiota namba sita.
SIMBA SC
Rais wa heshima wa klabu hiyo na na mwekezaji, Mohamed 'MO' Dewji, aliposti jezi namba sita japo aliifuta muda mfupi baadaye.
Mzabuni wa jezi, JayRutty akiwa kwenye kipindi cha michezo cha redio moja kubwa hapa nchini, alitumia muda mwingi kuijadili jezi namba sita.
Alisema wangeweza kutengeneza jezi maalumu yenye hiyo namba na kuwataka mashabiki wao wainunue kama sehemu ya kukusanya pesa kumpata namba sita huyo ambaye yeye alimuita X-Factor.
Matukio haya yakaamsha hisia kwa mashabiki wao na kujikuta wakitengeneza picha za mtandaoni zenye jezi namba sita na kujidai nayo.
YANGA
Kwenye akaunti rasmi ya klabu waliposti jezi namba 6 na kuendelea kuinadi kila siku. Wakitumia kauli mbiu ya Wat a plea, Yanga walitamba na sita utadhani tayari wameshakamilisha jambo.
Msemaji wao, Ali Kamwe akatamba mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, tayari wanaye namba sita waliyekuwa wakimuota.
MATOKEO YAKE
Baada ya yote haya zikafika siku zao huku kila mmoja akiwa hana namba sita na kubaki na mshangao.
Mbwembwe za Simba zikaishia kwenye mguu wa kulia Elvis Rupiah huku yule Wat a plea wa Yanga akageuka kuwa Tony Talasi wa Les Aigle du ambaye alifunga mabao mawili siku hiyo.