Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pata picha ‘Halftime Show’ kwenye Ngao ya Jamii

PUMZI Pict


FAINALI ya Kombe la Dunia 2026 ilikuwa ya tofauti kidogo kwa kulinganisha na miaka mingine na safari hii kulikuwa na tamasha fupi la muziki wakati wa mapumziko, kwa ajili ya kuburudisha wahudhuriaji na watazamaji.


Huu ni utamaduni mpya kwenye mashindano hayo na hata kwenye mpira kwa asilimia kubwa, lakini ni maarufu sana kwenye michezo ya kimarekani, kuanzia mpira wa kikapu, magongo, hockey na michezo yao yote maarufu.


Hata hivyo, tamasha kubwa zaidi hufanyika kwenye Super Bowl, mchezo wa fainali ya taifa ya soka la kimarekani ambao ndio mchezo unaopendwa zaidi nchini humo.

Katikati ya mechi hiyo kubwa ya mwaka, huwa kunakuwa na tamasha la muziki ambalo huitwa Half Time Show na wasanii wao wakubwa wa muziki hufanya onyesha la hali ya juu sana.

Utamaduni huu umekuwa maarufu kiasi kwamba kila baada ya tukio kupita Dunia nzima hujadili onyesha la muziki lilivyokuwa na kuongeza ufuatiliaji wa mchezo wenyewe na kuzidi kupata umaarufu duniani.

PUM 04

TUFANYE NA SISI

Tanzania tumejaaliwa kuwa na wasanii wa muziki wenye ufuasi mkubwa Afrika na muziki wetu unakubalika maeneo mengi katika kipindi ambacho mpira wetu pia unakua. Kumbuka pia ligi yetu ni namba sita Afrika na namba 54 duniani.

Vitu hivi viwili vikiunganishiwa matukio kama wanavyofanya Marekani na FIFA walivyojaribu kwenye Kombe la Dunia, vinaweza kutukuza kibiashara.

Agosti 12 kutakuwa na mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar ikiwakutanisha wakubwa wa mpira wetu, Yanga na Simba.

Hii ndio Super Bowl yetu, ndio mechi kubwa ya kufungulia msimu wa mpira ambao ndio mchezo namba moja hapa nchini.

Mamlaka zenye kuhusika, TFF na Bodi ya Ligi, zingejaribu kuja na wazo la kuandaa Half Time Show kwenye tukio hilo na kuwatumia wasanii wetu wakubwa.

PUM 02

Sasa hivi kuna matamasha makubwa ya miaka 30 ya Bongo Fleva yanaendelea nchini na moja wapo ya wadhamini ni Azam TV ambao pia ndio waoneshaji wakuu wa mpira wetu.

Siku ya Ngao ya Jamii, watu wa Bongo Flava wafanye tamasha lao pale uwanjani, hata kwa nusu saa tu...halafu mpira uendelee.

Mpira na muziki zote ni burudani na kwa hapa kwetu asilimia kuwa mashabiki ni wale wale, kuwawekea burudani ya pamoja ni kuongeza thamani ya tukio.

Wasanii wa muziki wamekuwa wakitumika kwenye mechi za mpira hapa nchini, hata fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB pale Pemba mwaka huu alikuwepo Ali Kiba.

Hata hivyo, onyesho lake halikuandalia kama Half Time Show, aliimba kabla ya mechi na ufanisi haukuwa wa ki-superbowl. Siyo suala tu la msanii kwenda kuimba...ni suala la msanii kwenda kufanya tamasha la kibabe.


UTAPENDA

Katika historia ya matamasha ya aina hii kwenye Superbowl, matatu yafuatayo yanatajwa kuwa ndiyo bora ya muda wote.

Prince mwaka 2007, Michael Jackson mwaka 1993 na Dr. Dre na marafiki zake mwaka 2022.


PRINCE 2007

Linatajwa kama tamasha bora zaidi la msanii mmoja peke yake kufanya halftime show katika historia, akiimba nyimbo zake maarufu kutoka albamu yake ya Purple Rain, Prince alimaliza onesho lake kwa kunyeshewa na mvua ya kutengeneza, kama jina la wimbo wake.

PUM 01

MICHAEL JACKSON 1993

Hapa ndipo palipojengwa msingi wa matamasha ya kisasa ya halftime show kwenye superbowl.

Wahusika waliimba nyimbo zilizobamba na kupendwa, tofauti na kabla ya hapo na wasanii waliimba nyimbo za mashairi magumu ya kufikirisha wakiwa na bendi za watu wanaotembea kama wanaandamana na mabango yao.

Michael Jackson alizichapa nyimbo kali kama “Billie Jean” na “Heal the World” na kutengeneza utamaduni mpya kabisa wa halftime show.

PUM 03

DR. DRE NA MARAFIKI ZAKE 2022

Hii ndio halftime show bora zaidi inayotajwa kihistoria na ilijaa majina makubwa yaliyokamua katika onesho lilinoandaliwa kitaalamu zaidi kuwahi kutokea. Ubunifu uliotumika kwenye show hii haujawahi kukaribiwa tena.


NA SISI TUNAWEZA

Mlete Diamond Platnumz afanye halftime show kama alivyofanya kwenye Africa Day Benefit Concert. Ile ilirekodiwa lakini siku hiyo aifanye mbashara pale jukwaani.

Mlete Dully Sykes afanye show ya pamoja na Mr. Blue na Joslin la wimbo wa Dhahabu. Mlete TID aimbe Nipe Nafasi na Fid Q. Mlete Ali Kiba aimbe na Bien.

Mlete Sugu aimbe Mambo ya Fedha na Lady Jaydee, au Wananiita Sugu na Stara Thomas. Mlete Mr. Paul aimbe Buzi na Inspector Haroun. Walete Daz Nundaz waimbe Kamanda.

Mtu anaweza kusema mbona nimetaja nyimbo za zamani sana...hapana.

Dr. Dre aliimba California Love, wimbo wa mwaka 1995 alioimba na Tupac.

Hizi nyimbo huleta msisimko wa aina yake unapozisikia na kuwaona wale wale walioimba, wanaimba tena.

Tafadhali TFF na Bodi ya Ligi. Fikirieni kuandaa Half Time Show kwenye Ngao ya Jamii.