Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usiichukulie poa CHAN 2024

POA Piict

Muktasari:

  • CHAN ni michuano inayofuatia kwa ukubwa ngazi ya timu ya taifa Afrika baada ya Afcon.

FAINALI za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN 2024) ufunguzi wake ni leo Jumamosi Agosti 2, 2025 na wenyeji Tanzania watacheza dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

CHAN ni michuano inayofuatia kwa ukubwa ngazi ya timu ya taifa Afrika baada ya Afcon.

Kwa tafsiri ya kawaida, Chan inahusisha timu za taifa zenye wachezaji wanaocheza ligi za ndani kwenye nchi husika, wakati Afcon ni mchanganyiko wa ndani na nje ikiwemo wanaocheza Afrika na mataifa ya mabara mengine.

“Kwangu mimi CHAN ni mashindano bora zaidi Afrika kwa sababu inalenga wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki katika nchi zao za asili. Inaonyesha hali halisi ya soka la Afrika, hasa katika ngazi ya ndani,” anasema Kocha Mkuu wa Niger, Doula Harouna.

Michuano ya mwaka huu inayohusisha nchi 19, Tanzania ni mwenyeji kwa kushirikiana na Uganda na Kenya na tamati yake ni Agosti 30 mwaka huu, fainali ikichezwa Kenya. Pia Uganda imepewa hadhi ya kuandaa mchezo wa timu kusaka nafasi ya tatu, hiyo ni baada ya Tanzania kufanya tukio la ufunguzi wa michuano hiyo.

Wakati wengi wakiichukulia poa michuano ya Chan, ukweli ni kwamba siyo ya kawaida kwani inahusisha watu wenye wasifu mkubwa katika soka.

Licha ya kwamba wachezaji kucheza kwenye ligi zao za ndani ikionekana hawana majina makubwa, lakini upande mwingine kuna makocha waliowahi kufanya makubwa na tutawashuhudia kwenye michuano hii.

Mbali na hilo, kuna nyota kadhaa wameng’ara wakipata madili makubwa ya kwenda kucheza nje ya Afrika kupitia michuano hiyo akiwemo Meschak Elia (DR Congo) na Ayoub El Kaabi (Morocco).

Kuna mambo mengi ya kuvutia kwenye michuano ya mwaka huu ikiwemo mabingwa watetezi Senegal kushiriki wakimjumuisha mchezaji mmoja pekee ambaye alikuwepo katika kikosi cha mwisho kilichoshinda ubingwa huo ambaye ni Serigne Moctar Koite. Mbali na hilo, kuna hawa jamaa wenye wasifu mkubwa wanaokuja kuonyeshaa umwamba wao.

PO 02

Benni McCarthy (Kenya)

Ni kocha raia wa Afrika Kusini ambaye amepewa jukumu la kuiongoza Kenya katika michuano hii huku timu hiyo ikipangwa Kundi A.

Kenya itafungua kampeni ya CHAN 2024 dhidi ya DR Congo, mechi ikichezwa Agosti 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Moi Sports Center uliopo Kasarani, Kenya.

McCarthy ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Afrika Kusini akiwa na mabao 31. Pia ndiye Mwafrika Kusini pekee aliyeshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, akifanya hivyo msimu wa 2003-2004 akiwa na FC Porto ya Ureno.

Hapo awali, McCarthy alifanya kazi kama kocha wa Klabu ya Cape Town City na AmaZulu zote za Afrika Kusini, pia akawa kocha wa washambuliaji katika kikosi cha Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England, kwa misimu miwili 2022-2023 na 2023-2024 chini ya Kocha Mkuu, Erik ten Hag.

PO 03

Avram Grant (Zambia)

Raia huyu wa Israeli amefundisha klabu tatu tofauti za Ligi Kuu England ambazo ni Chelsea (2007-2008), Portsmouth (2009-2010) na West Ham United (2010-2011). Licha ya kwamba hakuwa na mafanikio ya kubeba taji lolote kwenye klabu hizo, lakini aliweka alama ya kuwa Kocha Bora wa Mwezi Aprili 2008 Ligi Kuu England kipindi anainoa Chelsea.

Klabu zingine alizofundisha ni Hapoel Petah Tikva ya vijana (1972-1986), Hapoel Petah Tikva (1986-1991), Maccabi Tel Aviv (1991-1995), Hapoel Haifa (1995-1996), Maccabi Tel Aviv (1996-2000), Maccabi Haifa (2000-2002) hizi zote za Israel sambamba na timu ya taifa hilo kuanzia 2002 hadi 2006.

Zingine ni Partizan Belgrade (2012), timu ya taifa ya Ghana (2014-2017), na sasa Zambia aliyojiunga nayo mwaka 2022.

Mafanikio aliyokuwa nayo ni kushinda Toto Cup Leumit msimu wa 1989/90 na 1990/91 alipokuwa Hapoel Petah Tikva, pia akabeba ubingwa kama huo msimu wa 1992/93 na 1998/99 alipokuwa akiinoa Maccabi Tel Aviv.

Maccabi Tel Aviv akashinda tena ubingwa wa Liga Leumit msimu wa 1991/92 na 1994/95, Israel State Cup (1993/94).

Akashinda ubingwa wa Ligi Kuu Israel msimu wa 2000/01 na 2001/02 akiinoa Maccabi Haifa sambamba na taji la Toto Cup Al msimu wa 2001/02.

Pale Chelsea, alimaliza nafasi ya pili katika Kombe la Carabao msimu wa 2007/08 pia nafasi kama hiyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huo.

PO 01

Kwesi Appiah (Sudan)

Licha ya kwamba hakucheza soka nje ya Afrika, lakini amejijengea heshima kubwa sana kwao Ghana kwa kuwa kocha wa kwanza Mwafrika kuipeleka nchi hiyo kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 iliyofanyika Brazil.

Appiah ambaye alikuwa akicheza beki wa kushoto katika maisha yake ya soka, amepata mafunzo ya ukocha katika klabu kubwa England za Manchester City na Liverpool.

Akiwa anacheza soka, alipata mafanikio kwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Ghana alipokuwa akiitumikia Asante Kotoko katika mwaka 1983, 1986, 1987, 1988/89, 1990/91, 1991/92 na 1992/93. Pia Kombe la FA Ghana 1984 na 1989/90 na African Cup of Champions Clubs (1983). Pia mwaka 1982 akawa sehemu ya kikosi cha Ghana kilichoshinda ubinwa wa Afcon.

Katika kufundisha, aliiongoza timu ya vijana ya Ghana chini ya miaka 23 kubeba ubingwa wa All-Africa Games mwaka 2011.

Appiah anaiongoza Sudan iliyopangwa Kundi D na timu za Congo, Nigeria na Senegal, huku timu hiyo ikiwa na matarajio ya kufanya vizuri kwani tangu iliposhinda AFCON mwaka 1970 haijapata mafanikio makubwa.