Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unajua mabao mangapi yameondoka Bara? Soma hapa!

WAMESEPa Pict


JANUARI 31, mwaka huu, dirisha la usajili Ligi Kuu Bara linafungwa baada ya kufunguliwa Januari Mosi mwaka huu, tayari baadhi ya timu zimefanya usajili kuboresha vikosi.


Wakati timu zikipambana kuboresha vikosi dirisha dogo la usajili, kuna baadhi ya timu zimebomolewa na baadhi ya mastaa wamejikuta wanahama kutoka Ligi Kuu Bara kwenda mataifa mengine.


Dirisha hili limeibua vicheko na simanzi kwa baadhi ya timu, wengine wamekuwa na vicheko huku wengine wakiwa na huzuni kuondokewa na mastaa waliofanya kazi kubwa.

Licha ya baadhi ya timu kulazimika kufanya biashara ya kuuza wachezaji wao hao ambao walikuwa na michango mikubwa kwenye timu zao kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi lakini wengine walitoka kutokana na kumshawishiwa na madai makubwa ya fedha wengi wao wamesema na mabao na asisti.

Mwanaspoti linakuletea orodha fupi ya nyota waliohama na mabao kutoka Ligi Kuu Bara na kwenda mataifa mengine kuanzia Januari 2025 hadi Januari 2026.

WAMES 01

CHARLES AHOUA

Amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na CR Belouizdad inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria, inayonolewa na kocha mkuu wa zamani wa Yanga, Mjerumani Sead Ramovic.

Tayari alitimka Simba baada ya kuuzwa Belouizdad akiwa ameitumikia Simba kwa msimu mmoja na nusu na kuandika rekodi za aina yake katika timu hiyo kabla ya kuondoka mapema mwezi huu.

Ahoua msimu wa 2024/25 alitengeneza jumla ya pasi tisa za mabao na kafunga 16, hivyo alihusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba iliyomaliza ligi katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 78 baada ya mechi 30.

Katika michuano ya kimataifa ambayo Simba ilikuwa inashiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2024-2025, Ahoua alichangia mabao matano, baada ya kufunga matatu na kuasisti mawili, yaliyoiwezesha kufika hadi fainali baada ya miaka 32.

Ilichukua miaka 32, tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipocheza fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, dhidi ya Stella Abdijan ya Ivory Coast na kuchapwa jumla ya mabao 2-0, chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Abdallah ‘King’ Kibadeni.

Katika fainali ya msimu wa 2024-2025, Simba ilicheza na RS Berkane kutoka Morocco na kuchapwa ugenini mabao 2-0, Mei 17, 2025, huku marudiano visiwani Zanzibar, Mei 25, 2025, zikatoka sare ya bao 1-1 na kukosa ubingwa kwa jumla ya mabao 3-1.


STEVEN MUKWALA

Julai 2, 2024, Mukwala alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Asante Kotoko.Mapema mwezi huu ameondoka ndani ya timu hiyo baada ya kuuzwa Al-Nasr ya Libya ambayo ndio timu atakayoitumikia kuanzia sasa kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Simba imefanya biashara kwa kumuuza mshambuliaji huyo Al Ittihad ya Libya baada ya mapendekezo ya benchi la ufundi kutokuwa na mpango wa kuendelea naye akiwa amebakiza mkataba wa miezi sita baada ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja na nusu.

Mukala ambaye alipachika mabao 13 msimu uliopita licha ya kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza msimu huu ambao ameondoka akiwa ameitumikia Simba kwa nusu msimu hajawa na namba nzuri.

WAMES 02

ARTHUR BADA

Ni miongoni mwa viungo washambuliaji nora waliowahi kupita Singida Black Stars, Arthur Bada, ambae alikuwa na msimu bora sana katika timu hiyo, hadi hapo viongozi walipofikia uamuzi wa kumuuza JS Kabylie ya Algeria.

Bada raia wa Ivory Coast ambaye alipata uraia wa Tanzania alipokuwa akiichezea Singida Black Stars sambamba na Mohamed Domaro Camara na Emmanuel Keyekeh ambao Wizara ya Mambo ya Ndani iliwatangaza kuwa raia wapya Tanzania awali Yanga walimwitaji lakini mambo yalikwenda sivyo baada ya JS Kabylye kuweka dau nono mezani ili kumpata kiungo huyo ambaye sasa yupo Algeria.

Kiungo huyo akiwa Singida Black Stars aliingia kambani mara tatu huku akihusika kwenye kutengeneza mabao manane.


STEPHANE AZIZ KI

Ni kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso aliyeanza kuitumikia Yanga Julai 2022 akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Alijitengeneza jina kubwa Ligi Kuu Bara kutokana na mabao na michango yake ya kimchezo.

Ameitumikia Yanga kwa misimu miwili na msimu wake wa mwisho katika kikosi hicho ulikuwa bora na wenye kuacha historia na kumtoa nafasi moja kwenda nyingine.

Katika msimu wake wa kwanza Yanga SC alihusika na mabao 14 kati ya 56 yaliyofungwa na timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 74.

Kwa msimu wa 2024/25 mchezo wake wa mwisho ulikuwa dhidi ya JKT Tanzania alianza kikosi cha kwanza kwenye hatua ya nusu fainali na mwisho ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ulisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Ndani ya msimu huo Aziz Ki  alicheza mechi 23 ambazo ni Sawa na dakika 1814 alifunga mabao 15 katika mabao hayo alikuwa na hat trick moja na alihusika kwenye kutengeneza mabao manane, huku akifunga penati mbili kati ya mabao hayo 15.

Uongozi wa Yanga uliamua kufanya biashara ya kumuuza kiungo huyo ambaye tayari alijitengenezea ufalme ndani ya kikosi hicho katika klabu ya Whydad ya Morocco baada ya kuweka dau Nono mezani.

WAMES 03

CHE MALONE

Che Malone Fondoh  ni beki wa kati raia wa Cameroon ambaye alijiunga na Simba Julai 2023 akitokea Coton Sport ya Cameroon. Alikuwa mchezaji tegemeo katika safu ya ulinzi na mara nyingi alicheza kama sehemu ya kikosi cha kwanza akiwa Simba.

Che Malone, alitua Msimbazi misimu miwili iliyopita akitokea Coton Sport ya Cameroon na kutengeneza ukuta mgumu sambamba na Henock Inonga aliyetimka klabuni hapo na sasa akishirikiana na Abdulrazack Hamza na Chamou Karaboue ukuta ambao umeifanya Simba kuendelea kuwa imara na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Beki huyo wa kati licha ya kutokuwa na msimu mzuri kama ilivyokuwa msimu wake wa kwanza akiifungia Simba mabao mawili kwenye mechi 26 alizocheza kabla ya kusepa na kutua USM Alger.

Rekodi ya Malone imefikiwa na mbadala wake wa sasa ndani ya kikosi cha Simba Rushine De Reuck ameweka kambani magoli mawili kwenye michezo miwili ya ligi kuu na kuifikia record ya mtangulizi wake Che Malone ambaye msimu uliopita alifunga mabao mawili kwenye michezo 26.


GIBRIL SILLAH

Gibril Sillah alikuwa kiungo mshambuliaji tegemeo wa Azam FC (2023-2025) akitokea Gambia. Katika kipindi chake cha misimu miwili (2023-2025), alicheza michezo 68, akifunga mabao 21 na kutoa pasi 10 za mabao (assists).

Sillah ambaye alijiunga na Azam FC akitokea Raja Athletic aliondoka klabuni hapo Juni 2025 baada ya mkataba wake kuisha na baadae aliibukia Es Setif ambayo pia amevunja mkataba nayo sasa atakipiga amejiunga na Al Ahly Benghazi ya Libya kama mchezaji huru.

WAMES 04

LEONEL ATEBA

Nyota huyo aliyejiunga na Simba baada ya kuachana na USM Alger ya Algeria aliyojiunga nayo Januari mwaka huu akitokea Dynamo Douala.

FC ya kwao Cameroon, alitua ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Ateba aliyeitukikia Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja na kuifungia mabao 13 msimu uliopita na baadae aliondolewa kikosini kwa Msimbazi kufanya biashara ya kumuuza klabu ya Al - Shorta ya Irak iliyompa mkataba wa miaka miwili anaitumikia hadi sasa.

Ateba aliondoka Simba msimu uliopita baada ya kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza chini ya kocha Fadlu Davis ambaye pia kwa sasa hayupo tena Simba.


FABRICE NGOMA

Ngoma aliyejiunga na Simba, Julai 2023 akitokea Al Hilal ya Sudan, alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Simba aliyetoa mchango mkubwa kuiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024/2025.

Kiungo huyo mkabaji, licha ya uongozi wa Simba kupambana kumpa mkataba mpya kutokana na ubora wake akiifungia mabao 4 timu hiyo walipambana kutaka kumuongezea mkataba ilishindikana.

Kiungo huyo mkabaji ambaye amecheza timu nyingi bora kutokana na ofa kubwa aliyokuwa amewekewa mezani kutoka Al-Nasr ya Libya aliamua kujiunga na timu hiyo akiondoka akiwa mchezaji huru.

WAMES 05

KENNEDY MUSONDA

Msambuliaji huyo ameitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu amefunga mabao 34 na kutoa asisti 13 akitwaa mataji matatu ya ligi na FA matatu na ngao za jamii mbili.

Musonda akiwa na Yanga amepata nafasi ya kucheza na washambuliaji mbalimbali ambao walishaondoka ikiwa ni pamoja na Fiston Mayele, Jean Baleke ambao hawapotena Yanga wengine ni Clement Mzize na Prince Dube.

Msimu wake wa mwisho kabla ya kuondoka baada ya kumaliza mkataba wake mwisho wa msimu uliopita aliifungia Yanga mabao matatu Ligi Kuu Bara na baadae kuibuka Hapoel Ramat Gan Givatayim ambayo aliifuga mabao 5 katika mechi 22.


JHONIER BLANCO

Alisajiliwa kutoka Rionegro Aguila ya Colombia, alitarajiwa kuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, lakini ndani ya wana lambalamba alishindwa kumudu changamoto za Ligi Kuu Bara, akiondoka na mabao matatu na asisti moja.

Kushindwa kwake kutamba na Azam, kumeibua maswali kuhusu uwezo wake wa kuendana na mtindo wa soka la Tanzania, Tofauti na mchezaji mwenzake wa Colombia, Yeison Fuentes Mendoza ambaye amekuwa akitumika mara kwa mara. jambo ambalo liliwafanya viongozi wa Azam kuanza kujadili uamuzi wa kumwacha mshambuliaji huyo.

Akiwa Colombia mwaka 2023  akiwa na timu ya Fortaleza alifunga mabao 21 katika mechi 35 kabla ya kutua Rionegro aliyoipandisha daraja akiifungia mabao 19.