Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugumu ulipo katika kuisaka rekodi mpya CAF

NONDO Pict
NONDO Pict


HISTORIA itaandikwa kama klabu za Tanzania zitatumia vyema mechi za marudiano za CAF.


Ndio ni wakati mwingine wa rekodi kuandikwa na timu za Tanzania katika michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu.


Ni wakati wa bendera ya Tanzania kupepea Afrika kwa klabu zetu zote nne wikiendi hii kutokana na kuwa na nafasi ya kuandika historia ya kutinga makundi.

Ndio timu nne kati ya tano kwa maana ya Simba, Yanga, Azam FC na Singida Black Stars zipo katika nafasi nzuri ya kutinga makundi kwa mara ya kwanza. Timu nyingine ni KMKM ambayo inavaana na Azam leo Ijumaa zikirudiana baada ya mechi iliyopita mabahari hao wa visiwani Zanzibar wakipasuka mabao 2-0.

Yanga licha ya kupoteza ugenini kwa bao 1-0 mbele ya Silver Straikers ya Malawi bado ina nafasi ya kupindua meza, Simba iliyo na hazina ya mabao 3-0 iliyopata ugenini huko eSwatini ina kazi ya kumalizana na Nsingizini Hotspurs. Hizo ni mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Singida iliyolazimishwa sare ya 1-1 na Flambeau de Center ya Burundi na Azam na KMKM zenyewe zipo katika Kombe la Shirikisho Afrika.

NOND 04

Kutinga makundi kwa timu hizo itakuwa ni mara ya kwanza kama taifa kuingiza klabu nne katika michuano ya CAF, lakini itakuwa ni rekodi nyingine kwa Azam na Singida zikitoboa wikiendi hii.

Azam iliyoanza kushiriki michuano ya CAF miaka zaidi ya 10 iliyopita haijawahi kucheza hatua hiyo kabisa na msimu huu ipo katuka nafasi hiyo kutokana na matokeo iliyopata ikiwa chini ya kocha mwenye wasifu mkubwa Afrika.

Singida yenyewe inashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya CAF, ikitinga nayo itakuwa ni rekodi tamu kama iliyowahi kufanywa na Namungo misimu mitano iliyopita iliposhiriki kwa maravya kwanza na kufuzu makundi.

NOND 02

Hata hivyo, Namungo licha ya rekodi hiyo tamu ilichemsha kwa kushindwa kupata ushindi hata mmoja wala kufunga bao mbele ya Nkana FC ya Zambia, Pyramids ya Misri na Raja Casablanca ya Morocco.

Azam FC kufikia hatua ya makundi kitu ambacho kwa msimu huu kinaonekana kiko upande wao kuanzia hatua za awali aina ya wapinzani kulinganisha na nguvu na uimara wa kikosi chao.

NOND 03

Timu nyingine kwenye shirikisho Singida inaonekana pia kuwa kwenye nafasi nzuri baada ya mchezo wa kwanza ugenini kumalizika kwa sare ya goli moja moja, ukiitazama mechi iliyochezwa nchini burundi unaweza kuona bado kuna mechi ngumu mbele yao ila kinachonipa matumaini ni aina ya kikosi walichonacho benchi la ufundi pamoja na management chini ya mlezi wao  wamekua wakijaribu kuibadilisha timu kila msimu na kuifanya kua timu inayoimarika kiushindani na kwa uwekezaji huo ni dhahiri kwamba makundi shirikisho ni saizi yao

Simba kama wabeba maono wa taifa kwenye michuano ya kimataifa wao kuingia makundi tena sio habari kwao wakifaidika na nafasi wanayoishikilia kwenye ubora wa vilabu barani afrika kutokana na alama walizojikusanyia imepelekea kupungua kwa kiasi cha ushindani kutoka kwa wapinzani wao kwenye hatua za awali kutokana na chungu anachokaa wakati wa upangaji wa ratiba hata ukitazama matokeo ya mchezo wa kwanza kama sio heshima kwa mchezo wa soka tungeweza kuipitisha kabisa ila watabidi kupambana tena kutunza hazina waliyonayo ya kushinda mchezo wa kwanza kwa goli tatu ugenini.

NOND 01

Yanga kama bingwa kwenye ligi yetu bado kwenye michuano ya vipabu barani Afrika hajakua na hadithi ya kutisha japo kuingia makundi kwao ni lazima kama mabingwa wa ligi yetu kwa misimu mi nne mfululizo, wako kwa goli moja lakini wana nafasi ya kupindua meza kutokana na kikosi walichonacho bila kujali wako kwenye kipindi gani bender a ya nchi inapaswa kupepea na wanakua sehemu ya kuandika historia ya taifa hili kwenye soka barani afrika

Mungu ibariki Tanzania Mungu zibariki timu zetu