Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuzo ya Mzize CAF ilivyobeba matumaini mapya

NONDO Pict


WIKI iliyopita straika wa kimataifa wa Yanga, Clement Mzize alishinda tuzo ya Bao Bora la Mwaka la michuano y Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitia Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mzize anayeitumikia pia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars alishinda tuzo hiyo kupitia bao aliloitungua TP Mazembe ya DR Congo katika mechi ya raundi ya nne ya makundi ya msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

NOND 05

Katika mechi hiyo, Mazembe ilinyooshwa kwa mabao 3-1 baada ya awali kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani na bao hilo kutajwa katika mabao makali yaliyoingia fainali kabla ya Mzize kuibuka kidedea, japo hakuweza kuhudhuria sherehe za kukabidhiwa kwa vile anajiuguza.

Katika kipengele hicho cha bao bora, Mzize alikuwa akichuana na Ghizlane Chebbak, Abdellah Ouazane, Barbra Banda, Anas Roshdy, Asharaf Tapsoba, Calvin Fely, Ibrahim Adel, Jean Claude, Ndabayithethwa Ndlonolo, Refiloe Jane, Oussama Lamlioui na Soufiane Bayazid.

NOND 01

Hii ni mara ya pili kwa timu ya Tanzania kutoa mshindi wa tuzo hiyo, hapo kabla mchezaji nyota aliyekuwa Simba, Pape Ousmane Sakho alibeba tuzo hiyo takribani miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, Sakho ni raia wa Senegal, tofauti na Mzize ambaye ni Mtanzania.

Ushindi wa Mzize umekuja wakati mchezaji huyo akiwa majeruhi, lakini timu yake ikizidi kufanya makubwa katika michuano ya CAF ikiwa hatua ya makundi kwa mara ya tatu mfululizo kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kushinda kipengele cha Bao Bora katika michuano ya Caf sio mara ya kwanza mchezaji wa timu ya Tanzania, baada ya Sakho kufanya hivyo akiwa na Simba, lakini kwa Mzize inaweza kuwa na kitu cha ziada na kuleta athari chanya kwa vijana wengi.

NOND 02

Hii ni darasa tosha kwa wachezaji wengine wanaoibuka kwa sasa hasa wale wanaoijua historia ya Mzize miaka mitano nyuma na kuwafanya wapate matumaini mapya kupambania ndoto katika maisha bila kukata tamaa. Ni chachu kwa wachezaji hao kwa kuamini kwamba jitihada zikikutana na fursa zinabaki simulizi tu zenye kuvutia.

Miaka saba kama sio mitano iliyopita, Mzize hakuwa anafahamika katika tasnia ya soka sio la Afrika tu, hata hapa Tanzania, lakini nani asiyemjua kwa sasa na ni juzi tu kulikuwa na mijadala kuhusu ofa zilizokuwa zikimiminika mitaa ya Twiga na Jangwani klabu kadhaa zikimkata.

Historia ya Mzize inaweza kuibua matumaini mapya kwa vijana na hata wazoefu kwamba kila kitu tunachokiona kikitokea kwa wachezaji wa mataifa mengine hata kwa wachezaji wetu inawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu iwe kwa kushinda kama timu au kwa mchezaji mmoja mmoja.

NOND 03

Miaka mingi tumekuwa tukishuhudia klabu na wachezaji kutoka mataifa mengine wakiingia katika kinyang’anyiro cha kugombea tuzo barani Afrika, lakini leo hii tumekuwa tukishiriki hatua hizo na kushinda ila kupitia wachezaji wa kigeni na kwa wengi ilionekana kama haiwezekani kwa wazawa.

Bahati nzuri ni kwamba pazia la Watanzania kutwaa tuzo za CAF lilifunguliwa mapema kabisa na Mbwana Samatta ‘Samagol’ a.k.a Popat enzi akiitumikia TP Mazembe, lakini kwa Mzize ni deni kubwa kwake na Watanzania wataweka matumaini makubwa kwake na kumfanya abebe matarajio makubwa kupitia kwake, klabu na hata timu ya taifa.

Deni hilo kwa yakini linaweza kumuimarisha au kumdondosha sababu hatochukuliwa tena kama kama mchezaji chipukizi bali ni mbeba maono wa timu ya Yanga na Taifa Stars, huku vijana wengi wakimtazama kama mfano wa kuigwa kwenye kupambania ndoto zao.

NOND 04

Ndio maana naamini tuzo ya Bao Bora la Mwaka la CAF kwa Mzize ni darasa tosha kwake mwenyewe na hata kwa wachezaji wengine katika kupambana ili kufikia malengo na kutumia kila fursa wanayopewa.

Kila la kheri kwa Mzize, namkumbusha tu, safari ndio imeanza inaweza kuwa na vikwazo vingi, lakini anapaswa kuvivuka kwa ajili ya kundi kubwa la vijana wanaotumia hadithi yake kama njia ya kujenga ujasiri na kuamini jitihada zao iko siku zitazaa matunda kama hawatakata tamaa.